Mwandishi gani wa habari Tanzania ni wa kariba ya Mohammed Ali wa Jicho Pevu Kenya Rd?

Mwandishi gani wa habari Tanzania ni wa kariba ya Mohammed Ali wa Jicho Pevu Kenya Rd?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kwa sasa ni Mbunge wa Nyali huko Mombasa. Kabla ya kujikuta kwenye siasa, alikuwa ni Mwandishi machachari wa habari za kichunguzi zilizokuwa zikirushwa katika kipindi kilichopata umaarufu mkubwa kilichojulukana kwa jina la JICHO PEVU, na kurushwa na moja ya vituo vya runinga nchini Kenya.

Kwa sasa hajishughulishi sana na uandishi, labda kutokana na majukumu ya kisiasa.

Kipindi akiwa anafanya uandishi, alipata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Kenya kutokana na kuibua taarifa nzito nzito, ambazo zimekaa kiuchunguzi hasa. Mwandishi mwoga asingethubutu kuziweka wazi wala kuzichunguza habari kama hizo. Zingine zilikuwa zikiwagusa "vigogo" na viongozi wa Serikali. Alikuwa anauweza "ushushushu".

Alikuwa Mwandishi wa habari za kiuchunguzi aliyeitendea haki taaluma yake.

Kwa Tanzania, nani anayemfanania Mohammed Ali katika tasnia ya Habari?
 

Attachments

  • Jicho_Pevu_Promo(144p).mp4
    1.4 MB
  • JICHO_PEVU_Trailer_🎬____kifo_cha_Magufuli(144p).mp4
    2.1 MB
  • Jicho_Pevu__Bughudhi_La_Ugaidi_5(144p).mp4
    15.3 MB
Tanzania unauawa sasa hivi....walikuwepo wengi wazuri sana....Stan K aliuawa ....( Loliondo Gate)...na wengine....wengi ! Utaabdamwa sanaa....hadi mauti...@ Paskal anawajua wenzake
 
Ishu unamchunguza Nani? Kwa faida ya nani? Je unaowafanyia hiyo kazi wanaithamini Kwa kiasi Gani? Azory G alipotea akifanya uchunguzi, hata Chombo chake Cha Habari hakikuwahi kuipa uzito unaostahili Hilo jambo.
 
Back
Top Bottom