Sisi kama Maskani tukiangazia wanatuwinda, wametutumia mpaka mademu, kumeresist, wametutumia watu tumeresist, sasa hivi tunasikia kwamba wanatumia moja ya mfanyakazi wetu wanampatia pesa atoe taarifa za mgari yetu na wapi tunaishi na sisi tunasema acha waje, kama tulizaliwa siku moja tutakufa siku moja.
Mwandishi wa habari si mhalifu, na hatuwezi kuacha kusema ukweli, kama umeua tutasema umeua, hatuwezi kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa kusema vitu ambavyo hujafanya, yale tunayotangaza ni ya ukweli hakuna kitu ambacho tunatunga, kama umechaguliwa kwa asilimia , kwa nini sherehe ya uapisho ifanyike kwenye kambi ya jeshi wewe umechaguliwa na wananchi au umeiba kura?
So, tunawindwa kweli na tunasikia kuna mmoja hapo ashaingia nchini na anatuwinda na sisi hatuwezi kuogopa kama tumeandikiwa tutakufa tutakufa na hatuwezi kuogopa.