Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Watu watatu wamefariki dunia akiwamo mwandishi wa habari wa kujitegemea mkoani Mbeya, Furaha Simchimba katika ajali iliyotokea mkoani humo ikihusisha basi la Kampuni ya CRN na gari la Serikali.
Ajali hiyo imetokea leo Jumanne Februari 25, 2025 katika eneo la Shamwengo wilayani Mbeya ambapo inadaiwa basi lilikuwa likilipita gari la Serikali bila kuchukua tahadhari na kusababisha ajali iliyosababisha vifo hivyo na majeruhi saba.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Wilbert Siwa amethibitisha kutokea ajali hiyo akieleza kuwa kati ya majeruhi saba, wawili wapo mahututi na wengine wameruhusiwa.
Soma Pia: Mbeya: Watu watatu Wafariki na wengine tisa wajeruhiwa katika ajali ya gari na bajaji
"Vifo ni vitatu akiwamo mwandishi wa kujitegemea na wengine wawili ambapo tutaendelea kutoa taarifa kadri tunavyopata," amesema Kamanda Siwa.
Kwa upande wake Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani hapa, Christopher Uhagile amesema ajali hiyo imetokea wakati wakitoka kumsindikiza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhil Rajabu aliyekuwa na ziara mkoani humo.