Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,355
- 14,408
Kivipi???.Leta hoja ."Bwana alitoa, Bwana ametwaa" ni kama kejeli kwa wafiwa na wapendwa wa marehem.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kivipi???.Leta hoja ."Bwana alitoa, Bwana ametwaa" ni kama kejeli kwa wafiwa na wapendwa wa marehem.
Kwanini huwa mnawafanyia ibada sasa??.Tujifunze kwa msiba huu, tuache dhambi, sisi wakristo hatuombei marehemu maana baada ya kifo ni hukumu, mambo ya kuombea marehemu ni ibada za wafu ambzo Mungu anazipinga
Wewe jamaa ni Nanga sana,Hiyo sala inaitwaje?.Naona umejiyungia mwenyewe kwa nia yako ovu.Mungu anakuona hadi rohoni mwako.“Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, …..”
Au;
“Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,….. Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……”
Nk.
Mchumba wa mungu hapo ni nani?
Hapo nimemuona Bwana James Nhende mwandishi mkongwe ambaye aliwahi kua Mhariri wa Habari za Michezo katika gazeti maarufu wakati huo likitoka kila Jumamosi, gazeti la Mtanzania ambalo lilikua linamilikiwa na Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania JUWATA enzi za chama kimojaMwandishi wa Habari mkongwe ambaye amewahi kufanya kazi, sehemu mbalimbali na hatimae akafanya kazi UTPC chini yangu mimi, amefariki dunia jana asubuhi kwenye hospitali ya rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.
Mipango ya mazishi yake tutawaarifuni baadaye leo. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.
========
Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC) unasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa mfanyakazi wa UTPC, Jacob Kabili kilichotokea tarehe 29/7/2020 katika hospitali ya rufaa ya Bugando baada ya kuugua kwa muda mrefu.
View attachment 1521200
Marehemu Jacob Kambili enzi za uhai wake
View attachment 1521203
Mwandishi mkongwe Bw. James Nhende akizungumza jambo kuhusu namna alivyofanya kazi na Jacob Kambili mpaka kufikia kustaafu akiwa UTPC
Gazeti ni Mfanyakazi mkuu.Hapo nimemuona Bwana James Nhende mwandishi mkongwe ambaye aliwahi kua Mhariri wa Habari za Michezo katika gazeti maarufu wakati huo likitoka kila Jumamosi, gazeti la Mtanzania ambalo lilikua linamilikiwa na Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania JUWATA enzi za chama kimoja
Gazeti hili lilipata umaarufu sana kutokana na sababu kadhaa ikiwemo kutoa habari za tetesi lakini zenye uhakika za michezo ndani na nje ya Tanzania na yeye huyo James Nhende akiwa mstari wa mbele kufanikisha hilo hadi kufikia kuuza nakala zaidi ya laki moja pindi linapochapishwa. Jambo hilo lilikua ni rekodi
James Nhende alikua ni shabiki, mkereketwa, mfurukutwa na nazi wa kutupwa wa timu ya Yanga, Maulid Kitenge anasubiri saaanaaa. Ilifika kipindi Yanga ikipoteza dhidi ya Simba badala ya kuleta habari kamili kuhusiana na mechi husika yeye atakuja na takwimu za historia ya nani kamfunga mwenzake zaidi, tena hiyo ndio inakua habari inayoongoza!!!
Kuna wakati Zamoyoni Mogella alimtwanga makonde baada ya kumponda gazetini tena kwa lugha ya kuudhi kua kwenye mechi kati ya Taifa Stars dhidi ya Uganda Cranes eti Mogela alikua nyoronyoooooro kabisa na alisababisha Stars wapoteze mchezo. Watu wote waliamini alifanya hivyo sababu Mogela alikua mchezaji wa Simba!
Nhende alimfungulia kesi polisi Mogella ya shambulio la kudhuru mwili ingawa alikuja kuifuta mwenyewe baada ya Zamoyoni Mogellah "Golden Boy" kubadili matokeo kwenye mechi ya marudiano pale Nakivubo Villa kwa kupachika mabao mawili safi kabisa kati ya matatu walioshinda Stars na kusonga mbele kwenye hatua iliyofuata ya michuano ya kutafuta nafasi kucheza kombe la dunia
Anyways, huu ni uzi kuhusiana na msiba wa mwandishi Jacob Kabili, Mungu Amlipe mema yake. Hii ya James Nhende nimechomekea baada ya kumuona hapo kwa picha