TANZIA Mwandishi wa Habari wa siku nyingi, Jacob Kambili afariki dunia

Wewe jamaa ni Nanga sana,Hiyo sala inaitwaje?.Naona umejiyungia mwenyewe kwa nia yako ovu.Mungu anakuona hadi rohoni mwako.
 
Hapo nimemuona Bwana James Nhende mwandishi mkongwe ambaye aliwahi kua Mhariri wa Habari za Michezo katika gazeti maarufu wakati huo likitoka kila Jumamosi, gazeti la Mtanzania ambalo lilikua linamilikiwa na Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania JUWATA enzi za chama kimoja

Gazeti hili lilipata umaarufu sana kutokana na sababu kadhaa ikiwemo kutoa habari za tetesi lakini zenye uhakika za michezo ndani na nje ya Tanzania na yeye huyo James Nhende akiwa mstari wa mbele kufanikisha hilo hadi kufikia kuuza nakala zaidi ya laki moja pindi linapochapishwa. Jambo hilo lilikua ni rekodi

James Nhende alikua ni shabiki, mkereketwa, mfurukutwa na nazi wa kutupwa wa timu ya Yanga, Maulid Kitenge anasubiri saaanaaa. Ilifika kipindi Yanga ikipoteza dhidi ya Simba badala ya kuleta habari kamili kuhusiana na mechi husika yeye atakuja na takwimu za historia ya nani kamfunga mwenzake zaidi, tena hiyo ndio inakua habari inayoongoza!!!

Kuna wakati Zamoyoni Mogella alimtwanga makonde baada ya kumponda gazetini tena kwa lugha ya kuudhi kua kwenye mechi kati ya Taifa Stars dhidi ya Uganda Cranes eti Mogela alikua nyoronyoooooro kabisa na alisababisha Stars wapoteze mchezo. Watu wote waliamini alifanya hivyo sababu Mogela alikua mchezaji wa Simba!

Nhende alimfungulia kesi polisi Mogella ya shambulio la kudhuru mwili ingawa alikuja kuifuta mwenyewe baada ya Zamoyoni Mogellah "Golden Boy" kubadili matokeo kwenye mechi ya marudiano pale Nakivubo Villa kwa kupachika mabao mawili safi kabisa kati ya matatu walioshinda Stars na kusonga mbele kwenye hatua iliyofuata ya michuano ya kutafuta nafasi kucheza kombe la dunia

Anyways, huu ni uzi kuhusiana na msiba wa mwandishi Jacob Kabili, Mungu Amlipe mema yake. Hii ya James Nhende nimechomekea baada ya kumuona hapo kwa picha
 
Tarehe ya kifo sijaelewa
Mtu kafariki 29/7/2020 kuna tatizo kwenye uandishi au mimi nimechelewa kuona post (natumia Tecno Y3).

Mtoa tangazo la tanzia mie bado sijaelewa

Yote kwa yote (R.I.P)
Kazi yake Mola haina makosa
 
Gazeti ni Mfanyakazi mkuu.
Namkumbuka I. Washokera na vibonzo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…