BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Nimeona ujumbe huu ukisambaa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na picha husika, nikaona niusogeze hapa ili Wadau watie neno.....
Mimi ni Dickson Ng'hily Mhariri wa Biashara na Mkuu wa Kitendo cha Digital The Guardian
Wakuu hamjambo.. Nimekamatwa na Walimu wa Shule ya Msingi Kwembe, Kata ya Kwembe, Wilaya ya Ubungo wakaanza kunipiga na kisha wakaagiza Wanafunzi waanze kunishambulia kwa kunipiga baada ya kunikuta nikipiga picha Wanafunzi wanasomea nje na chini ya mti.
Baada ya wao kuniumiza wamenipeleka Serikali ya Mtaa, yakatokea mabishano wakitaka nifute picha nilizopiga ndio waniachie.
Walioona nimegoma wakaamua kunileta Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Ubungo. Wakaninyang'anya kitambulisho na simu, ila simu zilipokuwa zikipigwa walinipa nipokee, nikatumia muda huo kuwa nazituma sehemu picha bila wao kujua.
Baada ya mabishano marefu ambayo pia yalihusisha DAS ambaye naye aliingilia baada ya kupewa maelekezo na DC mbaye hakuwepo eneo la tukio, wakaniambia nifute picha ndio waniruhusu niondoke.
Hoja yao waliniambia nimepiga simu Watoto na nikiwa eneo la shule, nikawaeleza kuwa sikuwa eneo la shule, nilikuwa mbali kabisa na Shule na hata mtu akisema atambue sura ya mtoto au Mwanafunzi hawezi kumtambua kutoka na umbali.
Mimi niliamua kupiga picha kwa kuwa nimekuwa nikiona wanakaa chini ya miti mara kwa mara, hivyo nikachukua kwa umbali ili niweze kutumia kwenye matumizi yangu ya baadaye.
Wameniumiza na wameharibu simu yangu sehemu ya kioo lakini sina mpango wa kuwashtaki kwa kuwa naamini nilichokuwa nakifanya ni kwa ajili ya Taifa na faida kwa haohao Wanafunzi walioambiwa wanipige.
Tamko la THRDC ~ THRDC yakemea Mwandishi wa Habari kukamatwa kwa kupiga picha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwembe wakisoma chini ya mti
Majibu ya Serikali ~ Madai ya Wanafunzi kusomea chini ya mti Shule ya Msingi Kwembe (Dar), Serikali yasema walikuwa katika programu maalumu