Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mwandishi wa Jambo TV amejikuta kwenye wakati mgumu alipokuwa akimuhoji Katibu Mkuu wa Chama cha DP Abdul Mluya, muda mfupi baada ya Mluya ambaye pia ni Mwenyekiti wa umoja wa vyama 13 vilivyotoa tamko la kupinga maandamano yaliyoandaliwa na CHADEMA kumaliza kuzungumza na wanahabari Septemba 17, 2024.
Ilikuwa hivi; katika mkutano huo wa wanahabari waandaaji/wazungumzaji wakiongozwa na Mluya walikataa katakata kuhojiwa swali lolote, hata hivyo Jambo TV iliazimika kumfuata Mluya na kumuomba izungumzenae yeye binafsi (sio kwa umoja wao) na baada ya kumuomba sana ndipo akaridhia.
Soma Pia: Waandishi wawili wa Jambo Tv wakamatwa na Polisi Mbeya akiwa kwenye majukumu yao ya kikazi
Hata hivyo mahojiano hayo hayakufika tamati baada ya mwandishi wa Jambo TV kuhoji kuhusiana na sakata la Tundu Lissu kupigwa risasi, na mashaka ya CHADEMA juu ya vyombo vya uchunguzi nchini.