Mwandishi wa habari wa Marekani, Rob Finnerty wa kituo cha Newsmax, amelazimika kuwaomba radhi Wakenya baada ya matamshi yake kuhusu Nairobi kuzua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii.
Katika kipindi chake cha Oktoba 9, 2026, Finnerty alidai kuwa ongezeko la wahamiaji kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Amerika Kusini limechangia kuzorota kwa baadhi ya miji ya Marekani, akisema miji hiyo inaanza kufanana zaidi na Nairobi kuliko New York.
Kauli hiyo iliwakasirisha Wakenya wengi, waliojitokeza kwenye mitandao ya kijamii kupinga matumizi ya Nairobi kama mfano wa jiji lililodorora. Baadhi yao walichapisha picha na video za miundombinu na majengo ya kisasa ya Nairobi, huku wengine wakihoji kwa nini alilitaja jiji hilo ilhali hakuna Mkenya aliyekuwa miongoni mwa wahamiaji waliohojiwa kwenye taarifa yake.
Baada ya ukosoaji huo, Finnerty alitoa taarifa Oktoba 13, akikiri kuwa alikosea na kuomba radhi kwa watu aliowaudhi. Pia alisifu namna Wakenya wanavyoonyesha upendo na uzalendo kwa jiji na taifa lao.
Hata hivyo, tukio hilo limeibua mjadala mpana kuhusu namna baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa vinavyozitumia nchi na miji ya Afrika kama mifano ya umaskini, uchafu au kushindwa kwa maendeleo.