Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 450
- 3,368
Taarifa za ndani zinasema Mwandishi wa Habari wa Millard Ayo mkoani Arusha, Godfrey Thomas ameshtakiwa kwa makosa ya Uhaini na Uchochezi.
Pamoja naye, lipo kundi kubwa la vijana ambalo idadi yake haijafahamika rasmi, lakini wote kwa pamoja walipandishwa kizimbani siku ya jana, Novemba 6, 2025 na sasa wapo gereza la Kisongo.
Ikumbukwe alikamatwa mwanzoni kisha kuachiwa huru na sasa amekamatwa tena: GE2025 - Arusha: Mwandishi wa Habari ambaye pia ni Mmiliki wa Kusaga Tv na Mwandishi wa AyoTv wakamatwa na Polisi
Hata hivyo, inadaiwa boss wake hataki taarifa hizi zijulikane kwa umma.