Mwandishi wa Watetezi TV mbaroni kwa madai ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni juu ya watuhumiwa kulazimishwa kulawitiana Kituo cha Polisi

Naona katendewa haki kisheria kwa kuwa kwanza ameitwa kituoni, pili amehojiwa mbele ya wakili wake. Naamini siyo tu kwamba haki itatendeka bali itaonekana inatendeka. Kama ana vipicha vya hao kulawitiana ama confession yao kwamba wamelawitiana, basi anaweze ku prove mahakamani kwamba alichoandika/alicho ripoti ni sahihi.
 
Jeshi la polisi hua wanakurupuka na kukanusha kila kitu bila uchunguzi wowote, kuna uwezekano mkubwa kabisa tukio hilo ni la kweli kwasababu polisi wetu sio mara ya kwanza kuthibitika kuwa wamefanya vitendo vya kinyama,
tusisahau walivyowaua na kuwapora mali zao wale wafanyabiashara wa madini, taarifa zilipotoka awali walikanusha hivihivi na kudai waliouawa walikua majambazi.
 
Waliofanyiwa ukatili huo wahojiwe mubashara na vituo vya luninga ( television) ili Watanzania wajue nani anstahili kuadhibiwa.
 
Police tukubaliane mapema..tunaanzia kwenye uraia au turuke moja kwa moja kwenye uhujumu uchumi?
#MembeSemaNeno#
#MwagaPombe2020#
Nadhan kitaalam tungeanza kwanza na ya kukutwa na Meno ya tembo ili akipanda mahakamani ndo wanaikuta ya kutakatisha hela, waonaje hii mkuu.
 
Nimeikumbuika hii habari na nilijua tu italeta shida kwa muhusika.
Ila waandishi tungejiongeza. Ili kuepuka ugonvi na $ tungehamishia uchunguzi wetu kwenye mambo mengine. Kunguru mwoga.................
 
Hii habari niliiona ukienda you tube ya hao watetezi online TV ipo, huyu jamaa alikuwa anawahoji vijana waliofanyiwa hivyo vitendo viovu sasa, washitakiwa wameongea wenyewe jamaa yy katuhabarisha tuu, sasa sijui kosa Lake ni lipi yaani jeshi letu kwa kuficha maovu kisa kulindana ni suala linalotufanya tuendelee kutokuwa na imani nalo katika kulinda usalama wa raia
 
Kwa wenzetu yaani hapo ungeona umahili wa wapelelezi kwa kufichua uovu hata kama ni wa wakubwa zao yaani muovu ni muovu tu hata kama ni askari mwenzao, hivi hapa kwetu tumelogwa na nani, yaani A tunaita B na k tunaita W yaani ni Sanaa tu dah I au a sana aisee
 
Hivi wandishi wa habari wamejifunza kuandika uongo!
 
Serikali mpya, jeshi lile lile. Ilipaswa hawa ma igp wapya wakiingia na wao tusikie wanapanga safu zao upya, kuanzia ocs hadi rpc
 
Nadhani yeye hakutakiwa kukamatwa kwa kuchapisha au kusambaza habari hii.
Labda kama hakufuata taratibu za kuwapa polisi nafasi ya kuwahoji waeleze maoni yao walihusika vipi na tukio hili.

Kama aliwahoji na chanzo chake cha habari walalamikaji wanaonekana wakihojiwa basi wa kukamatwa ni walio lalamika kutendewa hilo jambo endapo tu polisi wana uhakika walalamikaji wasema na taarifa za tukio la uongo.

Kwa hili jeshi la polisi watazidi kijichafua na kuichafua serikali kuhusu ukandamizaji waandishi wa habari bila sababu za msingi. Kama taarifa za uongo wa kukamtwa ni wale walio zusha uongo ambao ni walalamikaji.

Sasa kama huyu muandishi au mtu yeyite aliwarubuni waseme uongo watajifunza na vijana wengine wataogopa kushiriki matukio kama hayo. Vinginevyo askari walio husika wasilindwe waadhibiwe kama kweli walifanya uhuni huo.
 
Ipo youtube mkuu, wanahojiws na huyu mwandishi na wanasema wao kuwa walilazimishwa kulawitiana. Kama ni uongo basi waongo ni wale vijana sio yeye
Waliofanyiwa ukatili huo wahojiwe mubashara na vituo vya luninga ( television) ili Watanzania wajue nani anstahili kuadhibiwa.
 

Aisee

Fvxk the regime!
 
Polisi wao ndio watuhumiwa halafu wenyewe wajichunguze?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…