Lowassa ndiye Don Corleone wa siasa Bongo. Yeye na Rostum.Pamoja na malengo mazuri na ushupavu anaokuwa nao Kubenea, lakini ukweli unabakia kuwa ana agenda ya siri dhidi ya Lowasa. Sioni ni kwa vipi Lowasa alistahili kubeba kichwa cha habari hii. Mi nadhani mwanahalisi wanaweza kupotosha umma kwa kuonyesha kuwa ndani ya nchi hi ufisadi=Lowasa. Wapo wengi mafisadi ambao bado wapo na nyadhifa zao ambao gazeti linaweza kuwavalia njuga, na si Lowasa tu ambaye by the way hayupo tena madarakani...
Mkandara........Mwandosya ni waziri pekee nchini (mwenye Uraia wa nchi mbili) aliyeletwa na Mkapa kinyume cha mipango ya wanaCCM - Rukwa, Mbeya..Na yawezekana kabisa uwezo wake ktk Uongozi unatishia mfumo na utaratibu mzima wa Ulaji Mbeya..Na kulingana na navyowafahamu mila na desturi za Wadanganyika wooote, chuki binafsi (inda) zinaweza kuwa sababu kubwa ya matukio yoote haya kwani mgeni yeyote unapoingia mjini toka nje, usipokwenda kuwatembelea (salimia) nyumbani kwa mtu/watu wanaokufahamu basi wewe unajenga chuki na Unalinga.
Asante Mkuu.
Hili bifu kati ya Kubenea na Lowassa (na swahiba mwenza Rostam) lina sababu yake, na labda nidokeze tu ninachokisikia. Unakumbuka kesi ya tindikali? Imefikia wapi?
Imekwama kwa sababu washukiwa wakubwa behind kumwagiwa Kubenea tindikali ni wawili hao, EL na RA. Imekwama kwa sababu mtuhumiwa mmoja muhimu haonekani mtuhumiwa ambaye ndiye mhusika mkuu wa shambulio hilo la tindikali dhidi ya Kubenea.
Inadaiwa kasafirishwa nje baada ya tukio kama ilivyogundua timu ya Tibaigana iliyopewa jukumu la kupeleleza kesi tukio hilo. Mafweza mengi yalitembea kwa polisi kufanikisha hilo.
Kwa uchache kabisa habari ndo hiyo. Fikiria mtu anataka kukupofua macho unamfanyaje? But dont quote me! Mwenye habari zaidi azitoe.
Kwa haraka haraka naona Mkandara kachanganya watu.
Kubenea pamoja na kuombwa, bado anaandika kuwa George Mwakalinga ni MWANAFUNZI.
Mtanzania, hebu mtumie ID yako ya HUAWEI huyu Kubenea.
Labda ndiyo hapo milele atafahamu kuwa wewe SI MWANAFUNZI TENA.
Hilo lilishasemwa hapa sana tu. Sasa kama hata hilo bado Kubenea halioni, habari yake nzima inaleta utata.
Ila tu si kuwa kila anachoandika ni UONGO. Si hapa JF mnasema "Hata saa mbovu pana wakati husema ukweli...?"
Kwa haraka haraka naona Mkandara kachanganya watu.
Kubenea pamoja na kuombwa, bado anaandika kuwa George Mwakalinga ni MWANAFUNZI.
Mtanzania, hebu mtumie ID yako ya HUAWEI huyu Kubenea.
Labda ndiyo hapo milele atafahamu kuwa wewe SI MWANAFUNZI TENA.
Hilo lilishasemwa hapa sana tu. Sasa kama hata hilo bado Kubenea halioni, habari yake nzima inaleta utata.
Ila tu si kuwa kila anachoandika ni UONGO. Si hapa JF mnasema "Hata saa mbovu pana wakati husema ukweli...?"
Nkwingwa........Tunakuhitaji Sikonge bana..........Said keshajichokea
Ikiwa ni kweli Mwandosya ni raia wa nchi mbili kama Mkandara alivyosema, anaruhusiwa na sheria kugombea uraisi na kuwa waziri wakati nchi yetu haina uraia wa iana hiyo? Na nchi ipi nyingine ambayo Mwandosya ni raia wake? Aliungwa mkono na watu wengi alipogombea uraisi 2005. Wangejua ukweli huo, kama ni kweli kwamba ni raia wa nchi mbili, wengi wao wasingemuunga mkono.
Nina wasiwasi sana na ukweli wa habari hii. Kubenea anatumiwa na kundi la Mengi na wafuasi wake akiwemo Dr. Mwakyembe.................
Kwa muda mrefu Mwakyembe anafanya juhudi kubwa kutumia Nipashe na Mwanahalisi kuwagonganisha kati ya Mwakipesile na Prof. Mwandosya.....................
Hawa watu wawili sio marafiki lakini pia sio maadui kama gazeti linavyotaka kuonyesha. Ila Mwakipesile na Mwakyembe ni maadui wakubwa.
Prof. Mwandosya alichukua uamuzi wa maana wa kutokumshambulia Mwakipesile waziwazi pamoja na kwamba alikuwa anajua kwamba aliachwa pale Mbeya ili amwangalie prof. Mwandosya.
Kwa taarifa yako, nyuma ya Dk Mwakyembe, yupo Mwandosya na Hilda Ngoye sasa kama Mwakyembe hakufyrahia elewa na Mwandosya= Ngoye nao hawafurahii.. Mwakyembe hakufurahia hilo, yeye alitaka kuendelee kuwa na mikiki mikiki kati ya hao viongozi ili ile vita yake na Mwakipesile nayo ipambe moto.
Mkuu, Siasa ni Unafiki. Bifu za Mwandosya zimekaa kisayansi sio kama za kina EL et al (Mwakipesile akiwamo) Na ndio maana Mwakyusa anatambua kuwa Mwandosya anamfitini asirudi bungeni ili nafasi yake aichukue Hilda Ngoye lakini huwezi kuwakuta Mwakyusa na Mwandosya wana bifu za waziwazi. Wanapanda gari moja, wanakula pamoja na wanatembeleana.mama yake prof. Mwandosya, mkuu wa mkoa alienda na prof alimpokea bila vinyongo vyovyote.
Alivyofariki mama wa Mwakipesile, prof. Mwandosya naye alienda kumwona.
Mwakyembe na Mwandosya ni MAADUI wakubwa wa Mtandao wa JK ambao Mwakipesile ni mmoja wao. Uadui wao hautaisha. Uliza kilichotokea wakati wa uchaguzi wa wajumbe ya NEC ya CCM kisha pima intensity ya mgogoro wao.na Mwakyembe ni maadui wakubwa.
Uongo uliokubuhu, fanya utafiti kisha futa kauli yako.za chuki na visasi ndizo hata zimesababisha kupungua sana kwa uhusiano kati ya Prof. Mwandosya na Dr. Mwakyembe. Inasemekana prof hapendi hizo siasa za jino kwa jino na anaanza kujiweka pembeni ili asionekane wazi kwamba yuko upande mmoja.
Alienda kijijini kwa Mwandosya na hii ilitokana na ombi maalumu la Mwandosya kwa Bosi wake ambapo mara ya kwanza Mwakipesile aliipunch lakini mara ya pili alichemsha.alivyoenda Mbeya katika sehemu alizotembelea na kufungua miradi ya maana ilikuwa jimbo la prof. Mwandosya. Sidhani kama itakuwa busara eti kumpeleka rais nyumbani kwa waziri? Ataenda nyumbani kwa prof kufanya nini?
Ni suala la muda tu, Mbeya moto ulishawaka siku nyingi, Kumbuka ugomvi uliokuwapo kati ya Mulla (Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya) na Mwandosya mwaka 2008.tujihadhari sana na hawa watu ambao wanataka mkoa uwake moto shauri ya visa vyao binafsi. Huyu Kubenea anatumika sana kuchapisha habari ambazo zinaandikwa na watu wengine na yeye faida kwake ni kuuza hilo gazeti lake.
Hayuko kimya kama unavyomfikiria, huyu bwana ni hatari. Anaendesha mapambano kisayansi na watu alionao wanaomsaidia vita sio aina ya MAKAMBA.Mimi ni mfuasi mkubwa wa prof. Mwandosya na naunga mkono strategy yake ya kukaa kimya na kufanya mambo kwa vitendo kule kwake. Hii inamjengea sifa mkoani na hata hao wanaotaka kumwondoa hawatafanikiwa.
Hapa kidoooooooooooogo umejaribu kuwa mkweli.Kyela Rhoda wala haungwi mkono na mkuu wa majeshi. General Mwamunyange ameamua kuwa pembeni kabisa inapokuja siasa za Kyela maana anajua madhara yake. Huyo Mwakalinga naye anatajwa kuwa mwanafunzi, mbona wote tunajua hapa kwamba ni mfanyakazi tena wa siku nyingi sana? Makosa mengine yanaharibu habari kabisa.