SoC02 Mwanga kwenye giza(tulipotoka si sawa na tulipo)

SoC02 Mwanga kwenye giza(tulipotoka si sawa na tulipo)

Stories of Change - 2022 Competition

Ahazy mhanga

New Member
Joined
Jul 23, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Julai Mwaka 1992 Tanzania iliutangazia ulimwengu kuwa itaanza uchaguzi mkuu ambao utashirikisha vyama pinzani(mfumo wa vyama vingi) na mnamo mwaka 1995 ndipo uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi ulipofanyika. Matukio hayo yote yamekuwa yakishuhudiwa na wananchi wa Tanzania kwa muda wa miaka 61 mpaka sasa tangu kupata uhuru ambapo wananchi walishuhudia kufutwa kwa siasa za vyama vingi chini ya uongozi wa aliyekua Raisi wa kwanza mwalim Julius Kambarage Nyerere aliyedumu madarakani kwa muda wa miaka 24, kisha siasa hizo zikarejeshwa katika kipindi cha aliyekuwa raisi wa pili Ally Hassan Mwinyi chini ya tume ya jaji Francics Nyalali, huku mwalimu Julius Nyerere akiwa mstari wa mbele kuunga mkono siasa hizo.

CHANGAMOTO
Moja kati ya changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi wa kwanza chini ya vyama vingi, ni kuwepo kwa kesi nyingi zilizojitokeza wakati wa uchaguzi na mwaka 1995 ambao ndio ulikua mwaka wa kwanza wa uchaguzi wa vyama vingi vya siasa ni mwaka ambao ulishuhudia kesi nyingi sana za watu kutokutendewa haki, huku kesi zaidi ya 128 zikifunguliwa kupinga matokeo na moja kati ya kesi iliyotikisa zaidi ilikuwa ni ya aliyekuwa mbunge wa Temeke Ally Ramadhan Kihiyo.

HITIMISHO
Sote tunakubali maendeleo hayana chama,lakini ili kuwepo na maendeleo ni lazima tukubali kuweka haki katika kipindi cha uchaguzi (kuwepo kwa tume huru) ili kuweza kusimamia haki za vyama na wagombea wake ili kukwepa lawama na mapingamizi wakati wa matokeo ya uchaguzi.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom