Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Wakati wa ukoloni kulikuwa na mzungu mmoja aliyeitwa Ronald De La Bere Barker. Kwa majina mengine Mtawa Maporini au Mzee Rufiji. Alikuwa anaishi kwenye mapori ya karibu na mto Rufiji. Aliandika vitabu vingi sana kuhusu maisha yake na mambo aliyoyaona. Moja ya kitabu hicho ni juu ya Mwanga wa Shetani uonekanao vilimani huko Kilwa. Kwa wenyeji wa huko, Mwanga huu bado unaonekana? Wataalamu, nini kinaweza sababisha mwanga kama huo?
KILWA Kisiwani, zamani za kale ulikuwa mji mzuri sana, hata katika hadithi za Kiarabu unasemekana kwamba ni mji mzuri kupita yote duniani. Waarabu na Washerazi waliishi katika mji huu wa zamani unaokumbukwa kidogo na waalimu wa historia. Nilitaka kusahau, hata Wareno nao waliishi katika mji huu pia. Mpaka hivi leo mna masalia ya ngome na misikiti mikubwa mikubwa. Majeshi ya kienyeji yaliushambulia mji huu kama walivyoushambulia mji wa Mombasa. Kisiwa kizima cha Kilwa Kisiwani kimezungukwa na ukuta wa mawe madhubuti kwa hadhari ya kushambuliwa na maadui. Kuta hizi au tuseme ukuta huo, ulichomoza mizinga iliyoelekea kila upande ambayo mingine mpaka hivi leo bado iko. Nimeiona. Biashara kubwa iliyousimamisha mji huu ilikuwa ni ya watumwa, gundi, nta, sandarusi, pembe na viungo vya chakula. Msafara wa meli au manowari utaenea bandarini kwake bila shaka yoyote. Nafikiri serikali ya kiingereza ilitaka kupafanya mahali hapa kituo kikuu cha manowari na meli katika Afrika ya Mashariki. Meli kubwa kubwa zinafika bandari hii mpaka hivi leo kutoka Amerika kuja kupakia mkoko, yaani magamba ya mkoko, boriti na kadhalika.
Kuna kigongo kama tuta kubwa lililotambaa toka hapo Kilwa Kisiwani mpaka Nyasa. Wenyeji wanasema kwamba hakuna hata mto au kijito kilicholikata tuta hili tangu lilipoanzia mpaka lilipoishia. Eti yasemekana pia kwamba Majerumani walitaka kujenga reli juu ya tuta hili. Wenyeji wa Kilwa ni wazungumzaji na wacheshi kwa upande wao. Walinihadithia jinsi hapo zamani mji wao ulivyokuwa Waarabu na Washerazi walipokuwapo na hivi sasa mji ulivyokufa kwa kuondoka kwao.
Nikawaomba wenyeji wale wanieleze habari za mwanga uonekanao juu ya kilima cha Mpara mara kwa mara ambao habari zake nyingi nimepata kuzisikia. Jinsi walivyonijibu hawakuonyesha dalili yoyote ya kuuonea ajabu mwanga ule kama nilivyohadithiwa mimi hapo kwanza. Walinijibu kwa kifupi na kurahisisha kila neno. Walikuwa wameuzoea mwanga ule ulioonekana hata na babu zao wa ubabuni.
Kweli kuna mwanga juu ya kilima cha Mpara uonekanao usiku na hasa siku za mvua mvua. Mwanga huu una nuru sana hata utadhani ni moto ukiwa kwa mbali; lakini si moto basi, kwani hakuna kinachoungua. Isitoshe basi unaweza kuuona mwanga huu ukiwa mbali kidogo na kilima chenyewe, lakini ukienda kuutazama huko huko kilimani huuoni kamwe. Watu wote walioko pwani au mahali pengine wanaweza kuuona wazi wazi isipokuwa wewe ulioko juu ya kilima hicho wanakouona mwanga huo watu walioko mbali nao. Basi imekuwa kama ni mazingaombwe tu. Mabaharia wa majahazini wanasema kwamba wao huuona mwanga huo juu ya kilima cha Singino badala ya Mpara wakiwapo majahazini mwao.
Bwana Shauri mmoja alipoona mwanga ule akadhani wenyeji wamevunja amri na wanachoma pori. Akatoka na motokaa yake mpaka kwenye moto aliouona. Kufika kule kweupe! Hakuna moto hakuna lolote. Wenyeji wakamwambia moto aliouona ulikuwa ni mwanga wa shetani, na kwa kuwa yeye ni Mzungu hatopata bahati ya kuuona tena.
Basi magharibi wenyeji wakanipeleka mahali ambapo ningeliweza kuuona mwanga mara ukianza. Tukakaa chini juu ya makuti ya mnazi tukiangaza macho yetu huko na huko tukijiburudisha na muono tuliouona. Tukavunja madafu tukanywa tukisubiri wakati wa mwanga unapoanza. Kusini yetu vipori vya mikoko katika fuko za Kilwa vilionekana rangi ya kijani bichi kabisa hata vikakaribia kufanana na rangi ya bahari katika ghuba ya Kilwa Kisiwani iliyokuwa kama kibuluu kijani. Nchi ilikuwa shwari na ya amani siku ile. Ilikuwa ni vigumu kusadiki kama bara ya juu mvua kubwa ilikuwa ikianguka kwa mawingu ya mvua na radi zilizomweka tulizoziona. Mara mmoja wetu kasema, "Tazama!".
Karibu ya kilima cha Mpara mwanga mweupe badala ya mwekundu ukang'aa, katikati yake kulikuwa na kiini chekundu kilichoonekana kama jicho la shetani gani sijui. Wenzangu hawakuuajabia mwanga ule kama nilivyouajabia mimi. Mimi ambaye kila mara huwatania sana wenyeji kwa kusadiki kwao mambo ya ushirikina, siku ile niliingiwa na woga wa kikweli kweli. Wale wenzangu wakaniambia kuwa mvua ikiwa inapiga mwanga ule huongezeka nuru yake. Bwana mmoja wa Kijaro aliniambia kwamba alipouona mwanga huu ulikuwa mwekundu kama moto. Na Bwana Shauri mmoja alipokuwa akimhadithia Bwana Gavana habari za mwanga huu, alisema kwamba yeye alipouona alidhani ni moto wa kawaida unaopita mwaka hata mwaka katika mapori ya Kilwa na penginepo.
Asubuhi yake nikashuka kilima cha Singino nikaenda Kilwa mjini kufanya kazi yangu niliyoiendea. Watu niliokutana nao nilipofika mjini tu, walikuwa wafanyi biashara wawili mmoja wa kihindi na mmoja wa kishami, na wote walikuwa viziwi kamili. Mfanyi biashara huyu wa kishami ana ndugu yake mjini Dar es Salaam mfanyi biashara mashuhuri sana naye pia ni kiziwi. Nafikiri kwinini ndizo zilizowaharibu masikio yao. Kwa kuwa hata yule boi aliyekuwa amekaa barazani pa duka naye alikuwa kiziwi, nikadhani watu wote wa Kilwa Kivinje wameingiliwa na ugonjwa wa uziwi. Bila ya fahamu nilipokwenda kwa Bwana Shauri Bomani kutaka anipigie muhuri meno yangu ya ndovu ili niweze kumuuzia yule Mshami, nikamwambia kwa sauti kuu na kwa makelele nikidhani naye ni kiziwi pia. Bwana Shauri alishtuka mno kwa ujeuri niliokuwa nao. Lakini baada ya kumtaka radhi na kumhadithia habari ya viziwi niliokutana nao akacheka sana na kunisamehe. Nasikia kwamba siku hizi Kilwa Kivinje kukiwa na mchezo wowote namna ya senema hawakosi kutia mchezo wa Mzee Baka na viziwi aliokutana nao Kilwa.
MWANGA WA SHETANI