Nasibu hemedi
Member
- Aug 27, 2022
- 11
- 4
Mimi ni kijana wa Tanzania mwenye umri wa miaka 28. Nimeona leo nizungumzie masuala yanayousu taifa letu au nchi yetu ya Tanzania kwa utafiti wangu nilioufanya ndani ya miaka 6 kwenye mikoa ipatao 7 ndani ya nchi yangu ya Tanzania.
Ninaposema mwanga wa Taifa kuna baadhi wa watu wanaweza wasielewe kuwa namaanisha nini. Kwanza ninaposema mwanga simaanishi mwanga wa taa kama za umeme au taa za mshumaa hapana mimi namaanisha mafanikio au vyanzo vya mafanikio ndani ya taifa letu.
Mwanga wa taifa ni ile hali ya taifa kuwa na nguvu kazi inayo weza kuleta maendeleo chanya ndani ya taifa letu mfano taifa la Tanzania.
Taifa letu la Tanzania linategemea vijana wa kike na wa kiume ili kuandaa na kujenga taifa bora la leo na kesho ndio ndio mana kuna shule za awali mpaka vyuo vikuu yote hii ni kuijenga taifa bora lenye mshikamano ulio thabiti.
Serikali yetu inatambua wazi kuwa taifa hujengwa na vijana wenye afya bora na wenye uchungu wa kupigania maslahi ya nchi kwa pamoja. Taifa linapo kosa vijana walio bora basi jua hio nchi inaangamia hatakama kwa muda huo ina viongozi walio bora kwakuwa watapo staafu hakutakuwa na kizazi bora cha kuendesha nchi.
Umuhimu wa vijana katika taifa.
(a) Kujenga taifa la kesho; vijana wengi ndio wafanya kazi katika maebeo mbalimbali na ndio walipa kodi wakubwa hivyo kupitia kodi zao na juhudi zao nchi inapata maendeleo chanya.
(b) Kulinda taifa letu; vijana ni walinzi sio kwa taifa tu hata kwenye familia zetu huwa tuna tamaduni ya kuwafanya vijana wetu kuwa walinzi kwa ajili ya kuiweka familia salaama l, hivyo vijana hulinda taifa letu mfano wanajeshi na polisi wengi wao ni vijana.
(c) Kuongoza taifa ketu; vijana wengi ni viongozi katika sehemu mbalimbali tukianzia kwenye familia zao, ikumbukwe vijana wengine ni wazazi nao wana watoto wanategemewa hivyo wanavyo kuwa bora kuongoza familia zao na watoto wao ndio tunapata viongozi wa badae walio bora zaidi.
Je, Nini kifanyike ili kupata vijana walio bora na wenye uchungu na taifa lao?
(a) Elimu; vijana ndio taifa la kesho hivyo lazima wapate elimu bora bila kubagua kwakua hakuna ajuae kiongozi wa badae ninani hivyo elimu bora kwa kila kijana ni muhimu kwa ajili ya nchi yetu.
(b) Huduma bora za afya; kijana ili aje kuwa bora lazima awe na afyq njema kwakua kama kijana asipo kuwa na afya njema hatuwezi jenga mwanga wa taifa ulio bora kwa sababu ni sawa na kuchukua kisu butu ili ukatie nyama utakata ila kwa shida sana.
(c) Chakula bora na mazingira bora katika ukuaji wao; chakula ni muhimu kwa kila kijana, nasio bora chakula hapana inatakiwa chakula kilicho bora. Kijana anapopata chakula bora hata marazi yanamuepuka na anakuwa na akili ilio komaa hata kwenye kutatua maswala yake binafsi bila papara na kwa umakini.
Je, Vitu gani sisi vijana tunapaswa kuvipiga marufuku na kuviepuka?
(a) Kuacha kutumia madawa ya kulevya.
(b) Kuacha tamaa za maisha kwa kutaka mali zisizo halali kwakuwa hii hufanya vijana wengi kuiba na kuuwawa taifa linapoteza nguvu kazi.
(c) Tuache imani za kishirikina; vijana wengi wanaamini udhirikina mfano kujiunga friimasoni kuwa utapata utajiri hii ni natharia ambayo wengi wao hawana uhakika hivyo huacha kujituna na kuzani watapata mali kwa njia ya ushirikina.
(d) Tuache kupenda mataifa ya wenzetu kuliko taifa letu; vijana wengi hukimbilia nje ya nchi mfano sauth Afrika wakiamini kule ndipo palipokuwa na furusa za kujenga maisha mwishoe wanaenda nchi za nje kukaa huko na kuacha taifa lao haliakuwa hata hapa nchini zipo furusa kama zile kule njee mwishoe wengi hupoteza maisha na kupotelea mbali.
Hasara ya kuwa na vijana wasio kuwa na uchungu na taifa lao.
(a) Kupata viongozi wazembe; kijana asio kuwa na uchungu na taifa lake huyo ni sumu kwakua atakapo pata nafasi katika taifa huwa ataumiza wananchi na kuangalia tumbo lake mwenyewe.
(b) Kuongezeka kwa uhalifu nchini kwetu; hii hutokea sawa wengine wana baka mama zao ili wapate utajiri wengine hukaba watu wengine kuuwa watu na kuwanyang'anya mali zao hii ni kutokana na kuwa na vujana wajina na wasio jitambua ni hasara kwa taifa.
Je, Nini Serikali ifanye kupata mwanga mzuri wa taifa letu?
(a) Kuboresha huduma muhimu kwa kila maeneo iwe kijijini na mijini.
(b)Viongozi kujali wananchi wao na kuwafanya kuwa familia moja.
(c) Wananchi kuwaunga mkono viongozi wao na kuwakosoa palee wanapo kosea bila chuki na ushawishi kutoka upande wowote.
(d) Kutunga sheria ya kuwapa bafasi vijana wa ndani pindi kunapo kuja muwekezaji yani 95% ya waajiriwa wawe ni wazawa na ajira zipitie serikalini moja kwa moja na mishahara ipitie serikalini moja kwa moja.
Mwisho nashukuru sawa wote walio soma nakala yangu nina imani kwa pamoja tutajenga taifa lililo bora na nawakumbusha vijana wenzangu hakuna binadamu mkamilifu kwa hio kukosea kupo tusiwalaumu sana viongozi wetu walio madarakani nao ni binadamu huenda na wewe ungekuwa kiongozi ungekosea zaidi.
Tuwaombee kwa Mungu na tudumishe umoja na mshikamano wa taifa letu.

Upvote
3