GE2025 Mwangwi wa Baragumu la NRNE bado unalitetemesha Taifa; ni sauti ya Mungu kwa watanzania, na Lissu ndio Nabii!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mikopo Consultant

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2024
Posts
2,375
Reaction score
4,784
Shikamooni Wajumbe!
Mlimsikia Mke wenu mkubwa?
Kaeni mkao kuyasikia ya Ukweni!

Kama ambavyo kuna watanzania wenzetu hatunao sasa, waliotamani kuona reforms za uchaguzi zikifanyika, lakini hawakulishughudia hilo likitokea kwenye maisha yao; yawezekana pia hata kizazi hiki kisishughuhudie hilo likitokea - chochote kinaweza kutokea. Hii haina maana ya kusema kwamba: Agenda ya 'No Reforms, No Election (NRNE)', haijafanikiwa kubadili upepo wa kisiasa na uwanda mzima wa sheria za nchi hii - ukijumuisha utendaji wa vyombo vya dola vinavyotafsiri sheria hizi, kwa mapana hayo.

NRNE imekuja wakati sahihi sana kwenye historia ya nchi yetu - ni kama vile Mungu alitaka kuzungumza na watanzania, na tumesikia; japokuwa waanzilishi CHADEMA walikuwa na maono ya kutumia kauli mbiu hii, ili iwafaidishe kwenye uchaguzi wa 2025; maono ya NRNE yamejikuta yanavuka nyakati na uwanda, na kujikuta yanapenyeza kwenye mifumo mingi ya nchi hii - nje ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Ndani ya chama tawala chenyewe - CCM, Tumeona mnyukano mkali wa hoja uliolenga kukosoa mchakato wa kisheria uliotumika kwenye uteuzi wa kugombea nafasi ya urais, mpaka sasa kwenye ubunge na udiwani; reforms ni dhahiri, imethibitika.

Japo hatujafika bado hiyo Octoba, kuona ikiwa uchaguzi utazuiwa au lah!; ni wazi kwamba ukifanya upembuzi wa NRNE, utagundua ya kwamba ni ajenda yenye mwangi mkubwa - 'a mover and a shaker'. Kila mtu sasa ana hamaki kwamba: 'We need reforms across the board'. Na hii ni mafanikio makubwa, ni unabii mkubwa umetimia ndani ya muda mfupi; Mungu amezungumza na watu wake, na tumesikia (Kwa tunaoamini Mungu).

Haya yote maana yake nini?

1. Agenda ya NRNE, japo ilikusudiwa kwenye uchaguzi wa 2025, ila imelichechemua taifa na imegusa hata pale ambapo haikutarajiwa. Mahakama inaanza kushituka shituka, vyombo vya ulinzi pia natumai vitakuwa vitakuwa vimeshituka, CCM wenyewe wameshituka - kurudia teuzi za majina ya ubunge na udiwani kuna maanisha ya kwamba sheria zao pia zina matege!, zinahitaji kunyooshwa. Wale vyama vya visabengo, wenye uchu wa madaraka na tamaa ya fedha - waliokubali kuubariki uporaji wa uchaguzi, ni kama nao hawaamini amini, wanalamba matapishi yao kwa kuikubali ajenda ya NRNE kisha wanaishia kuyatema, wamechanganyikiwa.

2. Tundu Lisu na CHADEMA wameshinda. Wameonesha wanawaweza kusimamia na kuzitetea ajenda zenye masilahi ya kitaifa bila kuongozwa na tamaa ya madaraka na kukubali kirahisi kushawishiwa kwa fedha na kuasi mrengo wa uma wa watanzania - kama walivyofanya watu fudenge na vitatange!

3. Ikiwa ujumbe wa Mungu tumeupata sawia, maana yake lengo la Mungu kwa Tanzania limetimia; maana yake, ni kwamba, hata kukaa magereza kwa Lisu, kwangu mimi sioni kwamba ni tukio lenye maana sana kama ambavyo inafikiriwa na wengi. Lisu anaweza kukaa gerezani kwa mda mrefu zaidi - yawezekana hata miezi 5 ijayo, haitanishangaza. Ni hii ni kwasaba mfumo wa chama tawala CCM, target yao ipo focused tu, kuona kwamba jambo la Octoba 2025 linatimia, 'by hooks or crooks'. Hii maana yake ni kwamba, tutegemee kuona CCM ikizidi kuboronga na kujikwaa kila baada ya hatua kuelekea kwenye jambo lao la Octoba 2025. CCM kujikaanga kwenye mafuta yake mwenyewe ni faida kwa wanaotaka kuona mageuzi ndani ya nchi hii, na NRNE ni hatua muhimu.​

4. NRNE ni kidonge kichungu kwenye utawala wa Rais Samia; nadhani binafsi atakuwa anahisi kwamba, yale maridhiano yaliyoasisiwa kati yake yeye na Freeman Mbowe, yangeweza kutatua vitu vingi vilivyotokea kwa haraka ndani ya miezi 12 iliyopita - ambavyo kiuhalisia vimechafua taswira yake. Ukianza na matukio ya utekaji, mauaji, uporaji wa uchaguzi serikali za mitaa, kukataliwa kwa Mbowe etc, yote haya unaweza kusema ni matokeo ya CCM kutokuyapa umuhimu, hicho kilichoitwa maridhiano. Na hii naichukulia kama mlio wa baragumu; kwamba, endapo 'dialogue' isipopewa kipaumbele, kinachofuata huwa ni 'chaos', na tumeshuhudia.

Wasioona umuhimu wa NRNE au kubeza harakati zake - kama ilivyokuwa kwa yule 'Kijicho Upembe' na wale wapambe wengine - walioiita NRNE, kwamba ni 'TAKATAKA', ni aina ya wanasiasa wanaoamini ya kwamba kila kitu kinatakiwa kuisha Octoba 2025. Hiyo ni static thinking, ndo maana wamerubunika kirahisi kuingia kwenye mtego wa uchaguzi, na kujikuta wameingia kwenye historia ya kubariki uporaji wa haki za watanzania, wamepoteza relevance kwa uma - wamekuwa maadui rasmi wa uma.

Long live NRNE!
MC
 
Naona ile 4R iliyotumiwa kumrubuni Kamanda aliyeangushwa kwenye nafasi yake aliyoitumikia kwa miaka zaidi 20, na yenyewe imejifia kifo cha mende. Porojo zote kwisha!

Kilichobakia kwa sasa ni mapambano kati ya haki dhidi dhuluma!
 
4R itakuwa imeuliwa kwa ushauri wa wenye nguvu huko CCM; siamini kama ni Rais Samia aliiua kwa utashi wake.

Yule Mugabe wa Machame kilichomuondoa, ni kuamini kwamba pesa ni kila kitu! Akajikuta anaingia kwenye uchaguzi bila hoja, akachezea kichapo.

Kwa maana hiyo huu mwaka umekuwa special sana, hii miezi 5 itakuwa na vihoja vingi sana
 
Shikamooni Wajumbe!
Mlimsikia Mke wenu mkubwa?
Kaeni mkao kuyasikia ya Ukweni!

Kama ambavyo kuna watanzania wenzetu hatunao sasa, waliotamani kuona reforms za uchaguzi zikifanyika, lakini hawakulishughudia hilo likitokea kwenye maisha yao; yawezekana pia hata kizazi hiki kisishughuhudie hilo likitokea - chochote kinaweza kutokea. Hii haina maana ya kusema kwamba: Agenda ya 'No Reforms, No Election (NRNE)', haijafanikiwa kubadili upepo wa kisiasa na uwanda mzima wa sheria za nchi hii - ukijumuisha utendaji wa vyombo vya dola vinavyotafsiri sheria hizi, kwa mapana hayo.

NRNE imekuja wakati sahihi sana kwenye historia ya nchi yetu - ni kama vile Mungu alitaka kuzungumza na watanzania, na tumesikia; japokuwa waanzilishi CHADEMA walikuwa na maono ya kutumia kauli mbiu hii, ili iwafaidishe kwenye uchaguzi wa 2025; maono ya NRNE yamejikuta yanavuka nyakati na uwanda, na kujikuta yanapenyeza kwenye mifumo mingi ya nchi hii - nje ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Ndani ya chama tawala chenyewe - CCM, Tumeona mnyukano mkali wa hoja uliolenga kukosoa mchakato wa kisheria uliotumika kwenye uteuzi wa kugombea nafasi ya urais, mpaka sasa kwenye ubunge na udiwani; reforms ni dhahiri, imethibitika.

Japo hatujafika bado hiyo Octoba, kuona ikiwa uchaguzi utazuiwa au lah!; ni wazi kwamba ukifanya upembuzi wa NRNE, utagundua ya kwamba ni ajenda yenye mwangi mkubwa - 'a mover and a shaker'. Kila mtu sasa ana hamaki kwamba: 'We need reforms across the board'. Na hii ni mafanikio makubwa, ni unabii mkubwa umetimia ndani ya muda mfupi; Mungu amezungumza na watu wake, na tumesikia (Kwa tunaoamini Mungu).

Haya yote maana yake nini?

1. Agenda ya NRNE, japo ilikusudiwa kwenye uchaguzi wa 2025, ila imelichechemua taifa na imegusa hata pale ambapo haikutarajiwa. Mahakama inaanza kushituka shituka, vyombo vya ulinzi pia natumai vitakuwa vitakuwa vimeshituka, CCM wenyewe wameshituka - kurudia teuzi za majina ya ubunge na udiwani kuna maanisha ya kwamba sheria zao pia zina matege!, zinahitaji kunyooshwa. Wale vyama vya visabengo, wenye uchu wa madaraka na tamaa ya fedha - waliokubali kuubariki uporaji wa uchaguzi, ni kama nao hawaamini amini, wanalamba matapishi yao kwa kuikubali ajenda ya NRNE kisha wanaishia kuyatema, wamechanganyikiwa.

2. Tundu Lisu na CHADEMA wameshinda. Wameonesha wanawaweza kusimamia na kuzitetea ajenda zenye masilahi ya kitaifa bila kuongozwa na tamaa ya madaraka na kukubali kirahisi kushawishiwa kwa fedha na kuasi mrengo wa uma wa watanzania - kama walivyofanya watu fudenge na vitatange!

3. Ikiwa ujumbe wa Mungu tumeupata sawia, maana yake lengo la Mungu kwa Tanzania limetimia; maana yake, ni kwamba, hata kukaa magereza kwa Lisu, kwangu mimi sioni kwamba ni tukio lenye maana sana kama ambavyo inafikiriwa na wengi. Lisu anaweza kukaa gerezani kwa mda mrefu zaidi - yawezekana hata miezi 5 ijayo, haitanishangaza. Ni hii ni kwasaba mfumo wa chama tawala CCM, target yao ipo focused tu, kuona kwamba jambo la Octoba 2025 linatimia, 'by hooks or crooks'. Hii maana yake ni kwamba, tutegemee kuona CCM ikizidi kuboronga na kujikwaa kila baada ya hatua kuelekea kwenye jambo lao la Octoba 2025. CCM kujikaanga kwenye mafuta yake mwenyewe ni faida kwa wanaotaka kuona mageuzi ndani ya nchi hii, na NRNE ni hatua muhimu.​

4. NRNE ni kidonge kichungu kwenye utawala wa Rais Samia; nadhani binafsi atakuwa anahisi kwamba, yale maridhiano yaliyoasisiwa kati yake yeye na Freeman Mbowe, yangeweza kutatua vitu vingi vilivyotokea kwa haraka ndani ya miezi 12 iliyopita - ambavyo kiuhalisia vimechafua taswira yake. Ukianza na matukio ya utekaji, mauaji, uporaji wa uchaguzi serikali za mitaa, kukataliwa kwa Mbowe etc, yote haya unaweza kusema ni matokeo ya CCM kutokuyapa umuhimu, hicho kilichoitwa maridhiano. Na hii naichukulia kama mlio wa baragumu; kwamba, endapo 'dialogue' isipopewa kipaumbele, kinachofuata huwa ni 'chaos', na tumeshuhudia.

Wasioona umuhimu wa NRNE au kubeza harakati zake - kama ilivyokuwa kwa yule 'Kijicho Upembe' na wale wapambe wengine - walioiita NRNE, kwamba ni 'TAKATAKA', ni aina ya wanasiasa wanaoamini ya kwamba kila kitu kinatakiwa kuisha Octoba 2025. Hiyo ni static thinking, ndo maana wamerubunika kirahisi kuingia kwenye mtego wa uchaguzi, na kujikuta wameingia kwenye historia ya kubariki uporaji wa haki za watanzania, wamepoteza relevance kwa uma - wamekuwa maadui rasmi wa uma.

Long live NRNE!
MC

View: https://www.tiktok.com/@legendatre/video/7507349701189078328
 
Nguvu ya Lisu ktk kila jambo inanikumbusha wimbo mmoja uitwao.....MAIDAS TOUCH.... everything I touch changes into gold.

Sijui uliimbwa na nani!!
 
Back
Top Bottom