Mwanjala atangaza mpango wa maboresho makubwa Uwanja wa Sokoine baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa MREFA

Mwanjala atangaza mpango wa maboresho makubwa Uwanja wa Sokoine baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa MREFA

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Baada ya kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya, Elias Mwanjala amewahakikishia wana Mbeya na wapenzi wa soka kiujumla kushirikiana na serikali ili kuufanyia marekebisho makubwa Uwanja wa Sokoine hususani eneo la kuchezea (pitch) kwani Uwanja huo si rafiki pindi kunapokuwa na timu nyingi Mkoani Mbeya.

Mwanjala ameyasema hayo Aprili 06, 2025 baada ya kutamatika kwa mchezo wa Ligi kuu kati ya Tanzania Prisons 1-0 Kagera Sugar uliopigwa katika dimba la Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mwenyekiti huyo ameonesha nia ya kuhakikisha timu za Mkoa wa Mbeya zinasalia ligi kuu, huku zilizo katika madaraja ya chini zinapanda na kuahidi kushirikiana na viongozi wengine wa serikali kufanya maboresho makubwa ya uwanja wa Sokoine.

Ni mapema hii leo Uchaguzi wa MREFA umefanyika ambapo wajumbe wamemchagua Mwanjala kuwa Mwenyekiti mpya kwa kura za ndio baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kurudisha majibu ya usaili kwa Mwanjala kukidhi vigezo huku mpinzani wake Sadik Jumbe kutokidhi vigezo.
 
Mwanjala huyu ni yule aliekuwa Traffic Police Dar kule Kimara akastaafu mwaka juzi akarudi kwao Kyela?
 
Back
Top Bottom