Kishimbe wa Kishimbe
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 5,566
- 5,477
- MWENYEWE ANAFIKIRI COMEDY, KWANGU MIMI LOVE STORY!
Tumsifu Yesu kristo wadau!
Bwana Yesu asifiwe wadau!
Asalaam aleykum wadau!
Inanibidi tu niwaambie yanayonisibu maana siwezi tena kukaa nayo peke yangu, maana yanawezanitoa roho!
Kuna dada mmoja, jina simtaji, maana mh!............ Dada huyo anacheza maigizo fulani ya comedy kwenye TV fulani nguli nchini, siitaji maana hata mia hapa nilipo sina! Comedy show yenyewe inaitwa MIZ****E. Swow ya kwanza nilicheka sana maana kwa kweli ilikuwa inachekesha mno, kama kawaida, maana kwa kweli muandaaji pamoja na wadau wa kipindi hicho kwakweli wanajituma vilivyo. Na hapa ninapoandaa uzi huu nimetoka kuangalia show yao ingine ya kusisimua na kuchekesha!
Yote hayo tisa, lakini kubwa zaidi ni kwamba 'I'M GRADUALLY FALLING, DEEPLY, IN LOVE WITH THE BEAUTIFULL LADY WHO IS ALSO A GENIUS COMEDIAN!'. Yaani, ndugu zangu, timetable ya hicho kipindi ipo kwenye viganja vyangu kwa ajili ya huyo dada tu na kila show inavyoendelea machoni mwangu huwa sijitambui kama naangalia comedy au njozi yangu ya mahaba mazito! Kwa kifupi nampenda mno huyo dada! KILA NIMUONAPO NAPATWA NA KIHARUSI CHA MAHABA!
Kama ameolewa nitajitahidi kumpenda na mme wake maana ukipenda boga penda na ua lake. WADAU NAOMBA MSAADA WENU WA MCHANGO WA MAWAZO MAANA SIJUI NIFANYEJE! Mwenye kuweza kuniunganisha naye, kama 'single', aje inbox!
Tafadhali asiogope avatar yangu, sifanani nayo kwa sura wala roho!