Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mahakama Kuu mkoani Mwanza, imemwachilia huru Daudi Kanyengele, baada ya kushinda rufaa aliyofungua kupinga kifungo cha miaka 30 jela, aliyohukumiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilemela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumnajisi binti wa miaka 5.
Hukumu hiyo iliyotowa Juni 23, mwaka huu katika tovuti ya mahakama hiyo na Jaji Mwanabaraka Mnyukwa ambaye alisema uamuzi huo ulitokana na ushahidi uliotolewa wakati wa kusikilizwa shauri katika mahakama ya chini.
Katika rufani hiyo, Kanyengele alisimamia katika hoja kadhaa ikiwemo kwamba mahakama ya chini ilikosea kisheria kumtia hatiani kwa kuwa hakukuwa na uthibitisho wowote wa kitabibu kwamba binti huyo aliingiliwa, pia mahakama ya chini ilikosea kumtia hatiani kwa kuwa mwathirika hakueleza kwa kina aina ya mwanga uliokuwepo kumwezesha kumtambua kwa kuzingatia kuwa tukio lilitokea usiku.
Pia alidai kwamba mahakama ilikosea kumtia hatiani kwa ushahidi wa binti huyo ambao haukuwa umethibitishwa na kwamba umri wa mtoto haukuthibitishwa badala yake mahakama iliangalia tu maumbile ya mtoto wakati kuna watu huwa wamethiriwa na umbilikimo.
Katika uamuzi wake Jaji Mnyukwa alisema msingi wa rufaa ni kwamba mrufani anasimamia hoja kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka na kumekuwa na ukiukwaji wakati wa kuendeshwa shauri hilo katika Mahakama ya chini.