Mwanza: Amchoma mkono Mwanaye kisa kudokoa Chainizi

Mwanza: Amchoma mkono Mwanaye kisa kudokoa Chainizi

Chainizi fungu 200, baba la ovyo kweli, hasa mtoto akale wapi? Huyo ni mkorofi wa asili tu.
 
Mh kanda ya ziwa hivi chainizii ni kitu ya kunyimana
 
Ni lana kweli,kijana wangu jana tu katafuna nusu kilo nzima ya kitimoto,
Kazuga kufichaficha ila mi najua kala kiasi gani.
Sasa utampiga?
Ni mwanao nikacheka tu kula kilichobaki basi hata sijauliza.
Mwanangu kala kitu changu hasa chakula.
Si chake nayeye pia.
Hapana adhibiwe sio vizuri kula chakula chote hichoo , kingine ni hivi usimuadhibu mtoto hadi kero unamuita unampiga kwa kiasi ila lazima umuadhibu maana atakuwa anafanya hivyo na mtakosa muelekeo, lazima achapwe ajue kakosa akitaka chakula asubirie kupakuliwa mezani au apewe kidogo au kitu kingine mpaka watu wote waje mezani .
 
JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia, Maneno Thomas (35) mkazi wa Chamagati, wilayani Sengerema kwa tuhuma za kumchoma mikono mtoto wake kwa maji ya moto baada ya kumtuhumu kudokoa mboga ya majani aina ya chainizi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Wilbroad Mtafungwa, ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 30, 2023, baada ya kutoka katika shughuli zake.

Mtafungwa ameeleza kuwa mtuhumiwa alipofika nyumbani kwake alimwambia binti yake aitwaye Prisca Maneno (11), apike chakula cha usiku ndipo alipoelezwa kuwa hakuna mboga, kwani ililiwa na mdogo wake Daniel Maneno (9), ambaye anasoma darasa la pili Shule ya Msingi Mtakuja.

"Maneno Thomas alishatengana na mkewe kutokana na vitendo vyake vya kipigo cha mara kwa mara na mwanamke aliamua kuondoka," amesema Mtafungwa.

Amesema mtuhumiwa aliwasha moto kisha kuchemsha maji yalipochemka, alimuita mwanae Daniel Maneno na kumwagia maji hayo katika mikono yake yote miwili na kumsababishia maumivu makali.

Anasema baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa aliamua kumfungia mtoto huyo chumbani kwake na wananchi wa eneo hilo walishtuka kutomuona mtoto Daniel siku mbili mfululizo, ndipo walipoanza kufatilia na kugundua amefanyiwa ukatili huo.

Imeandaliwa na Cyprian Magupa, Mwanza .

Sources Via Habari Leo
Kanda ya Ziwa si ndio Kuna sengerema? Ndio sababu watu wa huko wengi wao ni wasengerema 😂😂
 
Back
Top Bottom