Mwanza: aomba rift kwenye gari la shule na kuwateka watoto wa chekechea, ataka hela ili awaachie

Mwanza: aomba rift kwenye gari la shule na kuwateka watoto wa chekechea, ataka hela ili awaachie

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Amani iwe kwenu watu wa MUNGU MWENYEZI

Kamanda mtafungwa ndo kayasema hayo
Japokuwa maelezo ya kamanda hayajitoshelezi lakin ndo kasema hivyo
===============
Wanafunzi wawili wa Shule ya Blessing Modern iliyopo Nyasaka wilayani Ilemela jijini Mwanza wametekwa na kupelekwa kusikojulikana na mtu ambaye hajafahamika mara moja wakiwa kwenye basi la shule wakienda shuleni.

Wanafunzi hao ni Magreth Juma (8) mwanafunzi wa darasa la pili mkazi wa Hesawa Capri Point na Fortunata Mwakalebela (5) mkazi wa Bugando jijini humo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbdroad Mutafungwa amesema tukio hilo la utekaji limetokea leo Jumatano Februari 5, 2025 saa 12 asubuhi eneo la Nasa Drive Capri Point jijini Mwanza wakati wakiwa kwenye basi la shule Toyota Hiace.

Akitoa taarifa ya tukio hilo mbele ya waandishi wa habari, Mutafungwa amesema mtekaji huyo licha ya kutofahamika, alipewa lifti kwenye basi hilo la shule lililokuwa na wanafunzi sita (mmoja wa chekechekea na watano wa msingi) na matroni, kisha kufanya tukio hilo.
LONDON BOY
 

Attachments

  • Screenshot_20250205-223231.png
    Screenshot_20250205-223231.png
    218.3 KB · Views: 2
Kamata hiyo matron a dereva weka ndani? Yani wazazi walipie usafiri wa watoto wao halafu wewe utoe lift?

Halafu hapa kuna dots haziungi. Kama ni saa 12 asubuhi na watoto wamepanda bus kwenda shule na bus lina dereva na matron maana yake hapo ilitakiwa watoto washukie shuleni na sio sehemu nyingine.

Je huyo mtekaji ameshukaje na hao watoto kabla yakufika shule? Matron na dereva walishikiwa bunduki?

Hao wajinga wawili wafinywe waeleze watoto walipo.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣tatizo la akili.badala aende akateke sehemu zenye pesa anaenda kuteka watoto😳🙌🙌🙌😃😃😃
 
Dereva na Matron wamezingua kwanini umpe lift mtu usiyemfahamu, maana huruma yao imeleta zahama kubwa kwa watoto sasa

Huko walipo Bwana awalinde dhidi ya huyo haramia
 
Polisi ukiwaomba lifti hawakupi wanapita baru hata kama upo porini, iweje dereva wa wanafunzi atoe lifti kwa mtu asiyemjua kupanda gari la wanafunzi?
 
Kumbe gari la kubeba wanafunzi linatoaga lift kwa watu tena wasiowajua!!!
Dereva anaelewa mchongo mzima, wamlete stakishari atasema yote hadi ya ziada, matroni na yeye wampige ban hana weledi wa kazi.
 
Back
Top Bottom