Mwanza: aomba rift kwenye gari la shule na kuwateka watoto wa chekechea, ataka hela ili awaachie

Mwanza: aomba rift kwenye gari la shule na kuwateka watoto wa chekechea, ataka hela ili awaachie

Nahisi mtoa mada kasema kabisaa "Maelezo ya afande hayajitoshelezi"
Angeongezea tuu "Hayajitoshelezi na nusu"
 
Wametekwa watoto je matron na Dereva hawakutekwa? na kama ndio ilikuwaje watoe maelezo vizuri hao
 

Muktasari:​

  • Tukio hilo limetokea saa 12 asubuhi ya leo Jumatano Februari 5, 2025 eneo la Kapri Point jijini Mwanza baada ya mtuhumiwa kupewa lifti kwenye basi la shule lililokuwa limewabeba wanafunzi hao kuwapeleka shuleni.
Wanastahili adabu ya kifo ama kifungo cha maisha wakipatikana
 
Maoni binafsi:

1. Mtekaji movie zinamdanganya. Atakamatwa. Ata wazungu wenyewe kutoka for ramson money waliacha.

2. Matron na Dereva imekula kwao.

3. Naamini Askari wanajua wanachofanya. Watafanikiwa.

4. Mtekaji usiwadhuru watoto physically wala psychological. Wape chakula pesa yako utapata.

5. Case za utekaji wa aina hii uwa zinaisha vibaya sana.

6. Pole kwa wazazi na ndugu.

7. Sheria itungwe, kila school bus liwe na Camera.
 
Unatoaje lift kwa bus la shule?
Dereva nae ana kesi ya kujibu
Kazi yake ni kuhakikisha usalama wa watoto, kuwapeleka shule na kuwarudisha
Sasa inakuwaje unabeba stranger au anamjua na wamepanga haya
 
Kamata hiyo matron a dereva weka ndani? Yani wazazi walipie usafiri wa watoto wao halafu wewe utoe lift?

Halafu hapa kuna dots haziungi. Kama ni saa 12 asubuhi na watoto wamepanda bus kwenda shule na bus lina dereva na matron maana yake hapo ilitakiwa watoto washukie shuleni na sio sehemu nyingine.

Je huyo mtekaji ameshukaje na hao watoto kabla yakufika shule? Matron na dereva walishikiwa bunduki?

Hao wajinga wawili wafinywe waeleze watoto walipo.
Unaambiwa ni kawaida yao kupakiza abiria na wwnafunzi..na sio hao tu kuna baadhi ya school bus madereva wao wanapakiza abiria wanaokota buku buku hizo..wengine wanalipwa kwa mwezi
 
Unaambiwa ni kawaida yao kupakiza abiria na wwnafunzi..na sio hao tu kuna baadhi ya school bus madereva wao wanapakiza abiria wanaokota buku buku hizo..wengine wanalipwa kwa mwezi
Huu ni wendawazimu kabisa. Ina maana hakuna public transport
 
Back
Top Bottom