Wanajamvi habari zenu na Poleni na Majukumu, Leo nimekuja tofauti kidogo hivi mnaionaje kanda yetu kinachozalishwa na tunachorejeshewa na serikali,embu fikiria kutoka mgodi wa GGM ulipo mpaka pale Kakola ni kama 70km migodi miwili mikubwa sana lakini barabara ni vumbi vijiji vya huko maji tabu miundombinu hoi, kutoka kakola mpaka kahama km kama 75 nako Kuna Mgodi mkubwa miaka na miaka ndo juzi wamekumbukwa angalau lami, kutoka kakola mpaka mgodi mpya Nyanzaga ni kama 45 km tu nako hali ni tete sana, nenda shinyanga Almasi inachimbwa toka mkoloni yupo mpaka leo, Nenda Bunda hapo kuona wanyama ni nauli yako tu, Mwambao wa fukwe za ziwa Victoria salale ni kagera, Geita, Mwanza, Mara nafikiri na Simiyu, ilipaswa walau tuwe na mji au jiji moja kubwa la dhahabu kama kwingine wanakoita miji yao mara ya kibiashara, mara ya kitalii ilimladi tu wapate sababu za kupendelea huko, Rudi kwenye jiji letu la Mwanza figisu za wazi wazi yaani zile siasa za kizamani za viongozi kusema uongo ndio ziko huku, Mtu anakwambia soko kuu ni 93% toka December mpaka leo hata zabuni za kugawa vyumba hatujasikia, Limladi lenu la maji butimba limegeuka la kupigia picha maji hawajasambaza popote, Huo uwanja wa ndege ndio unatumika watu kujifua uwezo wao wa kudanganya, barabara zetu sasa nenda tu kisumu hapo mji population ndogo kabisa ila miundombinu babu kubwa, Huwezi kusikia Makao makuu ya Taasisi yoyote ya serikali ipo huku au inajengwa huku, Sijui kujenga chuo kikuu cha serikali hakuna hata tetesi, tunapata tabu cement tunanunua karibu mara mbili ya bei za wenzetu wa kanda zingine ila huwezi kusikia mpango walau wa kujenga kiwanda cha cement kanda ya ziwa, kiufupi wametudamp vibaya mno na ile kwamba ni jiji namba mbili sooni tunaenda kupokwa, je nini kifanyike?