Mwanza hii tabia ya kutulisha mbwa acheni

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
😡😡 Wakazi wa Mwanza, Mungu anawaona. Hii tabia iliyotamalaki ya kulisha watu kitoweo cha mnyama mbwa sijaipenda.

Tukio la kwanza lilitokea eneo maarufu Buswelu Centre, sehemu inayoitwa MSUKUMA PUB, kuna kaka pale anapika supu maarufu Mangi japo ni Mmeru anaitwa Mbise, wiki chache zilizopita alikamatwa usiku na askari wa doria akiwa na mzigo walipomtilia shaka na kumpekua akakutwa na VICHWA 4 (vinne) vya mbwa. Baada ya kubananishwa akakiri kuwa huwa anachanganya nyama ya mbwa na mbuzi, alikaa mahabusu siku kadhaa baadae wamemwachia anaendelea na biashara yake.

Tukio/matukio mengine ni kule sehemu za viwanja vya nane nane Nyamhongolo nako viliokotwa vichwa viwili (2) vya mbwa maeneo ya karibu na uwanjani, puuuuuuuuuuuuuuu!!! kumbe baadhi ya washenzi walikuwa wanachoma nyama za mbwa.

Tuhurumiane jamani, mbwa sio utamaduni wetu.
 
wewe nawe uko jijini mwwnza supu ya sato aliye nona ama supu yakuku wa kienyeji huzioni?
Samaki huku ni mlo wa kila siku wala sio kitoweo cha hamu. Tunawala sana hadi wanakinaisha
 
Ndio hivyo mkuu. Watu wanasaka hela kwa nguvu hadi wanatulisha mbwa, mwishoe tutapata magonjwa, mbwa wenyewe si ajabu wanamagonjwa hatarishi!!!!
 
😡😡 Wakazi wa Mwanza, Mungu anawaona. Hii tabia iliyotamalaki ya kulisha watu kitoweo cha mnyama mbwa sijaipenda.

Tukio la kwanza lilitokea eneo maarufu Buswelu Centre, sehemu inayoitwa MSUKUMA PUB, kuna kaka pale anapika supu maarufu Mangi japo ni Mmeru anaitwa Mbise, wiki chache zilizopita alikamatwa usiku na askari wa doria akiwa na mzigo walipomtilia shaka na kumpekua akakutwa na VICHWA 4 (vinne) vya mbwa. Baada ya kubananishwa akakiri kuwa huwa anachanganya nyama ya mbwa na mbuzi, alikaa mahabusu siku kadhaa baadae wamemwachia anaendelea na biashara yake.

Tukio/matukio mengine ni kule sehemu za viwanja vya nane nane Nyamhongolo nako viliokotwa vichwa viwili (2) vya mbwa maeneo ya karibu na uwanjani, puuuuuuuuuuuuuuu!!! kumbe baadhi ya washenzi walikuwa wanachoma nyama za mbwa.

Tuhurumiane jamani, mbwa sio utamaduni wetu.

Ila hakuna aliyedhurika sio?!!
 
Kuna mbwa wangu amepotea mwezi uliopita mpaka leo hajaonekana, iumbe haka kamtindo kameanza huku?
 
Back
Top Bottom