Mwanza imezizima wananchi wakesha kuusubiri mwili wa mpendwa wao hayati Magufuli utakaowasili saa 1:00 asubuhi!

Mwanza imezizima wananchi wakesha kuusubiri mwili wa mpendwa wao hayati Magufuli utakaowasili saa 1:00 asubuhi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Sijapata kuona heka heka za kiwango hiki katika jiji la Mwanza ambapo watu wamekesha kumsubiri mpendwa wao hayati Magufuli waweze kutoa heshima za mwisho.

Kwa kweli hayati Magufuli anakubalika kanda ya ziwa maana nimeshuhudia wageni kutoka pembe zote za kanda hii wakiwa tayari kumpokea, kumuaga na hatimaye kumsindikiza hadi Chato kipenzi chao.

Vituo vya mafuta viko busy kuuza maana kila mmoja ameshakaa mkao wa mapokezi, kuaga kisha msafara kuelekea Chato baada ya zoezi la kumuaga hayati Magufuli kukamilika katika uwanja wa CCM Kirumba.

Updates;
Uwanja wa CCM Kirumba umefurika, watu ni wengi kweli kweli na wote wakiwa na sura za huzuni na simanzi.

Kule kwenye mzunguko ambako wamekaa wananchi wa kawaida kulijaa tangu alfajili kabisa kadhalika jukwaa la viongozi limeshasheheni wahusika.

Mwili wa hayati Magufuli umeshawasili uwanja wa ndege wa Mwanza na sasa msafara umeanza kupita katika mitaa mbalimbali ya jiji la Mwanza na baadae kuelekea uwanja wa CCM Kirumba.
 
Mtu anayekubalika huitaji kumpigia kelele zote hizi, ukiona mtu anajisifu/kusifiwa kuwa anakubalika/kupendwa jua kuna tatizo sehemu.

Leo nimesikia eti wanampamba kuwa alikuwa mtu wa haki nikasema mhuuuu jamani tumfika huko!!!
 
Ndio kwanza saa 5 usiku ila mtoa mada anakwambia "watu wamekesha kumsubiri mpendwa wao hayati Magufuli waweze kutoa heshima za mwisho."

Nina wasiwasi Johnbaptist anaweza kua ndio Majaliwa maana sio kwa hizi propaganda.
 
Back
Top Bottom