Mwanza: Jeshi la Polisi latoa taarifa za uhalifu ikiwemo ulawiti na ubakaji pamoja na wanawake wanaojihusisha na ukahaba

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia jumla ya watu 91 wakituhumiwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya kihalifu yakiwemo ya ulawiti na ubakaji, wizi na wanawake wanaojihusisha na vitendo vya ukahaba hapa jijini.

Pia madereva Sita wa mabasi ambao watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kukiuka sheria za usalama barabarani.

Tukio la kulawiti na kubakaTarehe 07/11/2024 muda wa saa 7:00 mchana katika mtaa wa Kashishi, kata yaNyamhongolo, wilaya ya Ilemela, mwanamke ambaye jina lake limehifadhiwa kwasababu za kimaadili, mwenye miaka 68 alifanyiwa kitendo cha ukatili kwa kubakwa na kulawitiwa akiwa nyumbani kwa Atanas Michael Masubo.

Tukio hilo limetokea wakati mama huyo alipoenda nyumbani kwa Atanas Michael Masubo ambaye ni jirani yake, ambapo alimkuta anakunywa pombe aina ya konyagi ambaye alimkaribisha na kunywa pombe hiyo pamoja.Wakiwa wanaendelea kunywa pombe ndipo Atanas Michael Masabo alimuagiza binti wa kazi kwenda kununua pombe nyingine ili waendelee kunywa ndipo alipata mwanya wa kumuingilia mama huyo kimwili huku akimtishia kumuua kwa panga alilokuwa ameshika mkononi mwake.

Baada ya tukio hilo mama huyo alifanikiwa kukimbia na kutoa taarifa polisi ambapouchunguzi kuhusiana na tukio hilo ulianza mara moja na mtuhumiwa ambaye amefahamika kwa jina la Atanas Michael Masubo, miaka 65, dalali na mkazi wa Kashishi tayari amekamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la kikatili.

Uchunguzi umekamilika na jalada limepelekwa ofisi ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

IMG_20241113_222928_226.jpg

12.11.2024 usiku ilifanyika misako katika maeneo ya Buhongwa, kituo cha mabasi nyegezi, Mkolani, Mkuyuni, Liberty na Rufiji na kufanikiwa kukamata watu 90 wanaotuhumiwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya kijinai, katika kundi hilo kuna vijana 42 ambao wanaishi katika mazingira magumu ya mitaani ambao wamekuwa wakiwapora watu mali zao katika maeneo mbalimbali ya hapa jijini na wakipata fedha au mali za wizi wanazitumia kucheza kamari.

Watuhumiwa 48 kati yao wanawake 34 wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya ukahaba pamoja na matumizi ya dawa za kulevya.

Chanzo cha matukio haya ni kutafuta kipato kwa kutumia njia ambazo siyo halali nauchunguzi kuhusiana na matukio hayo unaendelea kwa tukishirikiana na wenzetu waustawi wa jamii na uchunguzi utakapo kamilika watachukuliwa hatua stahiki za kisheria.

Jeshi la polisi linaendelea kutoa wito kwa wazazi kuzingatia malezi mema ya watoto nakuwapa huduma muhimu ili wasiingie mitaani na kujikuta wanatumbukia katika matukioya kihalifu.

Pia tunawakumbusha baadhi ya wakina dada wanaojihusisha na vitendo vyaukahaba kuacha kufanya hivyo mara moja na badala yake watafute kazi halali za kujipatia kipato.

Kuhusu wanaume wanaochochea biashara hiyo ya ukahaba kwa kununua huduma ya mapenzi kutoka kwa wakina dada hao kuacha mara moja, misako dhidi ya watu hao wanaojihusisha na ukahaba itaendelea kutokana na matukio hayo kuwa na uhusiano na matukio mengine ya uhalifu.

Usalama barabaraniJeshi la polisi mkoa wa Mwanza limeendelea kutoa elimu kwa kuwataka madereva wa vyombo vya moto na watumiaji wengine wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuacha kufanya matendo hatarishi yanayoweza kusababisha ajali.

Wapo baadhi ya madereva hususani wa magari ya kubeba abiria wameendela kupuuza elimu hiyo wanayoipata kutoka kwa askari wa usalama barabarani na kufanya makosa hatarishi ambayo yanaweza kusababisha ajali, makosa hayo ni:-kupita magari yaliyo mbele yao bila kuchukua tahadhari (wrong overtakeking), kuzidisha abiria, dereva kuendesha gari akiwa amelewa, Kuendesha gari kwa njia ya hatari na kuhatarisha usalama wa watumiaji wengine wa barabara na kuendesha gari kwa mwendo kasi.

Kutokana na matendo hayo jeshi la polisi limeamua kuchukua hatua kali dhidi yao ili kuwakumbusha madereva wengine wanaopuuza elimu inayotolewa na jeshi la polisi na kuvunja sheria za usalama barabarani kwa kuwafungia leseni zao za udereva kwa kipindi cha miezi mitatu na kuwataka warudi vyuoni kwa mafunzo, madereva hao ni:-1. Abas Hamis Said, miaka 38, dereva, na mkazi wa Shinyanga aliyekukuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T.665 DQZ aina ya Yutong bus mali ya kampuni ya Ally's bus akiwa amelewa.

2.Gereon Edward Luyendela, miaka 53, dereva na mkazi wa Shinyanga aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T.357 DXS aina ya Golden Dragon mali ya kampuni ya Ally's bus alikamatwa kwa kosa la kuendesha gari kwa njia ya hatari na kuyapita magari mengine sehemu iliyokatazwa bila kuchukua tahadhari.

IMG_20241113_222928_679.jpg
 
Ukahaba nao ni uhalifu? Kumbe siku hizi

Hao ni watoa huduma siyo wahalifu

Na huduma hiyo ni biashara ya kitambo sana kabla ya wana wa Israel kwenda kanani
 
C

CCM wananifurahisha sana.
 
Sijaona Igogo, Kishiri, hizo ndio anga za wahalifu
 
Back
Top Bottom