Nchi hii sijui walioko madarakani watajitambua lini. Kwamba jiji la Mwanza limetumia bilioni 1.4 kugharamia timu ya Pamba?
Aibu naona mwenyewe. Hawa watu wana malengo gani na wananchi maskini?
Kuna kipande cha kama mita 500 hivi cha lami kutoka Buhongwa kwenda Bulale jijini humo, ambacho ujenzi wake umekwama kwa mwaka sasa, baada ya kuweka vifusi na kuiacha kama ilivyo.
Ingawa mahitaji ya barabra ni karibu kila eneo la mji huo, ni aibu kugharamia timu ya mpira kwa fedha za umma, huku ukiwaacha wananchi wakikosa huduma muhimu.
Kuna kituo cha Afya hapo Bulale, kinahudumia hadi wakazi wa wilaya jirani ya misungwi, magari ya kubeba wagonjwa yanahangaika na mashimo, kumbe 1.4 bilioni imegharamia timu!