DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafungwa, amewahakikishia wananchi usalama na kuwataka kushiriki shughuli za kisiasa bila hofu yoyote, kwani Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limeimarisha ulinzi katika maeneo yote.
Kamanda Mutafungwa ameeleza hayo Oktoba 18, 2025 katika Mwalo wa Kijiweni, Kata ya Chifunfu, Wilaya ya Sengerema, wakati akitoa elimu ya ushirikishaji jamii katika kuzuia uhalifu, ikiwa ni wiki moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu 2025.
“Kwa kipindi hiki cha kampeni kilichobaki, tunawahakikishia hakuna mkutano wa kampeni ambao hautalindwa. Mpango kazi wetu upo imara, jitokezeni bila hofu yoyote. Jeshi la Polisi lipo tayari kuhakikisha mnakuwa salama,” alisema Kamanda Mutafungwa.
Ameongeza kuwa: “Hakuna mtu atakayejitokeza kufanya vurugu katika mikutano hiyo. Atakayejaribu atadhibitiwa kwa mujibu wa sheria. Kazi yenu ni kutuunga mkono kwa kuwa watulivu na wasikilizaji ili kurahisisha majukumu yetu.”
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kijiweni, Fravianus Miyango, amesema maeneo ya mialo yamekuwa na changamoto nyingi, lakini kwa elimu waliyoipata kutoka Jeshi la Polisi, wataendelea kushirikiana nalo kikamilifu.
“Maelekezo yote yaliyotolewa tutayafuata. Uchaguzi utakuwa wa amani. Ninatoa wito kwa wananchi tulinde amani yetu, tusipoteze amani kwani ni kitu cha muhimu sana,” alisema mkazi wa Kijiweni, Riziki Mzizi.
Naye, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Sengerema, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Kulwa Misogalwa, ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kutimiza haki yao ya kikatiba, akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi lipo tayari kuwalinda ipasavyo.
"Wewe Mwananchi toka kifua mbele nenda ukapige kura. Katimize wajibu wako na haki yako kikatiba sisi tuko nyumayako na tuyakulinda kweli kweli" amesema Misogalwa