Pre GE2025 Mwanza: Katibu wa UVCCM Sengerema aonya makada wa CCM ambao wameanza kuhujumu mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Sengerema amewaonya baadhi ya viongozi wa jumuiya wanaotumika kupanga safu za wapiga kura wa maoni ndani ya CCM, akisema wanakiuka taratibu za chama hicho.

Ametoa wito kwa viongozi hao kuheshimu misingi ya chama iliyowekwa na waasisi wake na kuacha tabia zinazoweza kuvuruga umoja na mshikamano ndani ya CCM.

Soma pia: Pre GE2025 Mwenyekiti wa CCM Morogoro awapiga biti kali wagombea walioanza kampeni kabla ya muda uliopangwa

Kauli hiyo aliitoa wakati wa maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika Kata ya Igalula, ambapo jumuiya hiyo ilisherehekea siku hiyo kwa shughuli mbalimbali.

Huyu babu ni under 35? CCM kwa utapeli
 
Mbona Samia kavunja kanuni kujiteua bila hata ya kujaza fomu kwenye mkutano maalumu na mmefyata mkia?
 
Back
Top Bottom