Responded HOJA Mwanza: Kuna kero sugu ya maji. Wananchi tumechoshwa na visingizio

Responded HOJA Mwanza: Kuna kero sugu ya maji. Wananchi tumechoshwa na visingizio

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

seneni

Member
Joined
Jul 28, 2023
Posts
13
Reaction score
9
Hali ya maji katika Jiji la Mwanza inazidi kuwa mbaya! Mfano ni Nyegezi, ambako mitaa mingi imekaa takribani mwezi mzima bila maji. Hata mgao uliokuwepo umetoweka! Baadhi ya wananchi wanalazimika kuchota maji mitaroni. Hivi tunasubiri mlipuko wa kipindupindu?

MWAUWASA, VISINGIZIO VITAISHA LINI? Kila siku bomba limepasuka, mashine imeharibika au umeme umekatika. Cha kushangaza, viongozi wa Wizara wanapofanya ziara, maji yanapatikana; wakiondoka, tatizo linarudi! Hivi maji ni kwa ajili ya wananchi au ziara za viongozi?

37960.jpeg

37961.jpeg

37965.jpeg

37963.jpeg
Mabadiliko ya uongozi na ziara za viongozi bado hazijaleta suluhisho la kudumu. Wananchi wamechoka!

Ushauri wangu: Serikali ifungue fursa kwa sekta binafsi kushiriki katika uzalishaji na usambazaji wa maji. Mfumo wa sasa unahitaji mabadiliko ya msingi.

MWANZA TUNATAKA MAJI KWENYE MABOMBA, SI VISINGIZIO KWENYE VYOMBO VYA HABARI!

Pia soma ~ MWAUWASA: Huduma ya maji imerejea Nyegezi, kulikuwa na changamoto Oktoba 13 hadi 20, 2026
 
Back
Top Bottom