Mwanza: Machinga wasema awamu ya tano hawakusumbuliwa kama sasa

Mwanza: Machinga wasema awamu ya tano hawakusumbuliwa kama sasa

Wamachinga wa Mwanza waliandamana leo kupinga maamuzi ya uongozi wa soko la makoroboi la kuwahamisha

Wamachinga hao wametaka ujumbe umfikie Rais Samia kuwa wananyanyasika na kama wanataka kuharamisha umachinga basi wawatafutie kazi nyingine za kufanya
View attachment 2510525

Wanatema nyongo juu ya wakubwa kutumia mapesa ya walipa kodi vibaya, kutumia ma V8 n.k Naona somo limeaanza kuwaingia juu ya matumizi ya anasa na wizi ktk serikali ingawa hata wao machinga kukaa mitaani bila kupangwa pia ni kosa kisheria.

Lakini ujumbe uwafikie serikali kuwa sasa raia wanaona dhahiri tofauti ya walionacho na wasiyo nacho huku walionacho badala ya kupata utajiri na maisha ya anasa kwa kupitia shughuli halali, wananchi wanaona wanaibiwa kilicho chao halali na wakubwa wachache serikalini.
 
Kwani lazima waishi mjini?
Waende shamba kuna maeneo makubwa sana.
Sawa boss Ila kwa Maoni yangu kutokana na nilichopitia kufikia hapa mafanikio ni bahati tu na wakati wa Mungu ni wakati sahihi na maishani kuna kupanda na kushuka,nakuombea uje ushuke Mungu apate kukuonesha watu wa Chini wanapitia nin kuweka chakula mezani🙏
 
Wanatema nyongo juu ya wakubwa kutumia mapesa ya walipa kodi vibaya, kutumia ma V8 n.k Naona somo limeaanza kuwaingia juu ya matumizi ya anasa na wizi ktk serikali ingawa hata wao machinga kukaa mitaani bila kupangwa pia ni kosa kisheria.

Lakini ujumbe uwafikie serikali kuwa sasa raia wanaona dhahiri tofauti ya walionacho na wasiyo nacho huku walionacho badala ya kupata utajiri na maisha ya anasa kwa kupitia shughuli halali, wananchi wanaona wanaibiwa kilicho chao halali na wakubwa wachache serikalini.
Sasa kwann hawakwenda kuponda nyumba za hao viongozi unao waita waporaji badala yake waende kuponda mawe na kupora maduka ya walala hoi wenzao ambao nao yananyonywa na kama wao.
Hii tabia ya kutumia visingizio visio kuwa maana kuhalalisha uhalifu haikubaliki.

Hao wapuuzi walio fanya vurugu wasakwe na watiwe adabu.
 
Back
Top Bottom