KERO Mwanza maji yanatoka mara moja kwa wiki tena usiku wa manane au mchana. Tunashindwa kuhifadhi maji ya wiki nzima

KERO Mwanza maji yanatoka mara moja kwa wiki tena usiku wa manane au mchana. Tunashindwa kuhifadhi maji ya wiki nzima

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaiomba JamiiForums kutusaidia kupaza sauti kwa idara ya maji MWANZA (MWAUWASA)kwani ni mkoa ambao pamoja na kua na ziwa lakini maji yanatoka Jumatano au Alhamis pekee tena either usiku wa manane au mchana kitu ambacho inakuwa vigumu kwa kila raia kumudu kuhifadhi maji kwa week nzima, na imekuwa ni kama sheria kwetu hapa mtaani.

Pia soma
- MWAUWASA: Mwanza hakuna changamoto ya uhaba wa huduma ya maji, mteja mwenye changamoto awasiliane nasi
 
Mamlaka ya maji Mwanza ilishasema tatizo la maji Mwanza ni la mtu mmoja mmoja.
 
Kwa hiyo waishio Mazoo kwenye ziwa Victoria hawana tofauti na wale wa mikoa yenye ukame na shida ya maji!?
 
Watu wa mjini, fanyeni kama wale watu wa Nyikani Ngorongoro.

Mmelalamika vya kutosha, mmepuuzwa vya kutosha na sasa mnatakiwa kupiga kambi ya maandamano ya amani mbele ya ofisi za umma kudai haki yenu, ninyi walipa kodi ndiyo ma-boss.
 
Jamiii forum ipi? Hii inayofuta thread ambazo zinaiponda serikali
 
Nazidi kuomba jamii forum itusaidie kupaza sauti huku mwanza idara ya maji safi na taka wilaya NYAMAGANA mkoani MWANZA Mtaa wa NYAHINGI tunateseka sana maji yanapanda kwa siku moja tu kwa week nzima
Tunaiomba serikali kuliangalia hili kwan ni mkoa wenye ziwa jirani why tuteseke hivi???
 
Sisi tunaokaa Capri point maji yapo kila siku sijui wewe unakaa sehemu gani?

kama ni nje ya mji hamia mjini hakuna shida hizo.
 
Kuna nchi ni jangwa kabisa lakini wanapata maji na hawajawahi kulalamika kukosa
Sisi sio kingine bali ni akili hakuna tu
Unaishije na ziwa kubwa hivyo ulilolikuta ili ulitumie halafu unakuwa kama mnyama
Ujinga mzigo sana kwa kweli
Watasema hela zimepigwa la hasha ni akili nzito
 
Wakazi wa mbezi huku mageti na maeneo ya karibu kama muhimbili wamemkosea nini mama mwezi Wa pili hawana maji eti ni sababu za kisiasa
 
Haya ndiyo mambo ya kuungana wote na kuandamana bila kujali vyama .
Maji ni uhai .
Serikali yoyote isiyoweza kutoa huduma ya maji kwa wananchi wake ni serikali isiyojali uhai wa watu wake .

Wanakimbilia miradi ya kitapeli lakini miradi ya maji yanayotokana na mito ,maziwa na hata kujenga mabwawa kwa ajili ya uhai wa wananchi inasuasua na kuifanya iwe ni sehemu ya kampeni za kisiasa .

Nilishangaa juzi Mama mkubwa akizindua mradi wa maji wa kule Kilimanjaro .
Ule mradi ulianza kwenye kampeni za mwaka 2010 . Mbunge wa wilaya ya Mwanga wakati huo Profesa Maghembe akapewa mpaka Wizara ya maji . Wananchi wakiaminishwa kuwa Kufikia 2015 maji yatakuwa kama mafuriko wilaya za Mwanga na Same. 2015 kampeni za uongo zinaendelea maji yakiwa agenda .2020 zinaendelea ,maji yakawa ni agenda . Sasa ni 2025 ,maji kwenye majimbo hayo bado ni agenda .
Maji ni uhai ,serikali haijali uhai wa wananchi wake.
Wanaharakati na wanasiasa wapo kimya wanasubiri maandamano ya kudai tume huru peke yake . CCM inapata kiburi cha kuendelea kuwahadaa wananchi kuwa wao wanaahidi maji sio katiba kwani maji ndiyo maendeleao wanayotaka kusikia wananchi na sio katiba .
Kwa hiyo ni vyema sasa wanaharakati wahalasishe maandamano ya wananchi kudai huduma muhimu kama maji ambayo ni muhimu kwa uhai wa viumbe vyote ili CCM ikose pa kujificha na kuhadaa watu .
 
Kwani mpaka leo maji ni kero huko Mwanza?
 
Back
Top Bottom