Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 ahukumiwa adhabu ya kifo kwa kuwaua watu wawili kwa kukusudia

Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 ahukumiwa adhabu ya kifo kwa kuwaua watu wawili kwa kukusudia

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Mahakama Kuu Mwanza imemhukumu adhabu ya kifo mfanyabiashara wa kampuni ya mabasi J4, Jumanne Mahende (45) baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kuwaua watu wawili kwa kukusudia. Jumanne alikuwa akikabiliwa na Kesi ya mauaji namba 131 ya mwaka 2015

Anadaiwa kuwa Julai 13, mwaka 2015, saa 4 usiku, aliwaua kwa risasi, Ali Mohamed, fundi ujenzi wa Igoma wilayani Nyamagana na Claude Sikalwanda wa Nyasaka, Ilemela, Mwanza.

Kwa mujibu wa RPC Mwanza, Mkumbo alisema Saa 4 usiku Julai 13 mwaka 2015, mkurugenzi wa kampuni ya mabasi J4 Express akiwa anajiandaa kufunga ofisi yake, alikutana na watu wawili Ally Mohamed (35) na Claude Sikalwanda (35), ghafla ukaanza mzozo uliopelekea Luhende kuwapiga risasi na kufariki papo hapo.

Kwa upande wa ushahidi, mke wa Marehemu Ally Mohamed, Donatha Gabriel na Aziza Sikalwanda ambae ni dada wa marehemu Claude Sikalwanda waliiambia Mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 13 mwezi 7 mwaka 2015 siku ya tukio la mauaji lilipotokea marehemu waliwaaga kuwa wanaenda kuonana na bosi wao ambaye ni mtuhumini.

Inspekta Benidict Manyanda ambae ni shahidi namba tatu katika kesi hiyo aliiambia Mahakama kuwa siku ya tukio alifika eneo la tukio ambapo alikuta miili miwili ya marehemu ikiwa chini na baadae kuipelekea hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Pia soma > Mmiliki wa mabasi ya J4 apiga wawili kwa risasi
 
Duh! Very sorry for him! Ukisikia hasira hasara ndio kama hivi.
 
Mwenye picha yake aweke.
Maana kuja siku niko ibadan kanisa be Geita.
Akaja mkaka akatoa ushuhuda kuwa ni mmilili wa mabus ya J4 ule ushuhuda nikiri tu niliona ni usanii maana ulikuwa ni shuhuda hizi za kisasa tunazozijua.
Siku 2 mbele niko Hafsa Restaurant napishana nae wakati alisema pale akishtuka tu kumsalimia mtumishi. Anaendelea na safari ya kuonana na mabilionea wenzake.

Sasa nataka picha yake nifanye conclusion ni yeye kweli au tapeli tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hasira hasara . Lakini wale jamaa walikuwa wapigaji sana. Na Mimi ni mhanga wa mmoja wao . Yalikuwa matapeli wakubwa.
J4 hasira zimemponza [emoji40]

Sent using Jamii Forums mobile app
majamaa yapi? funguka Mkuu kesi imashaisha
fundi mwashi Ally Mohamedi na mwenzake Shekalwanda ndio wakamtapeli Jambazi au sijakuelewa
maana inasemekani Marehemu walikuwa wakimdai J4 kiasi cha 25milioni
naona amewazika na kuwazika kabisa wasiwepo duniani
 
Na mabasi yake yalishafutika barabarani hayapo tena.

Ila pesa ni mwanaharamu, ilikuwa huyu bwana akiletwa mahamakani kuna watumishi fulani wa kitengo fulani cha kuwalinda watuhumiwa, walikuwa wanapewa pesa kidogo, then mke wa J4 anajifanya amepakatwa anamlisha mumewe chakula kumbe mzee anafungua suruali anapiga kimoja
Ukwaju karibu Mwanza, hahahahah
 
I see bila Shaka wewe Ni mtu karibu Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na mabasi yake yalishafutika barabarani hayapo tena.

Ila pesa ni mwanaharamu, ilikuwa huyu bwana akiletwa mahamakani kuna watumishi fulani wa kitengo fulani cha kuwalinda watuhumiwa, walikuwa wanapewa pesa kidogo, then mke wa J4 anajifanya amepakatwa anamlisha mumewe chakula kumbe mzee anafungua suruali anapiga kimoja
Ukwaju karibu Mwanza, hahahahah
Eti ñini!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila pesa ni mwanaharamu, huyu bwana akiletwa mahamakani kuna watumishi walikuwa wanapewa pesa kidogo, then mke wa J4 anajifanya amepakatwa anamlisha mumewe chakula kumbe mzee anafungua suruali anapiga kimoja
Ukwaju karibu Mwanza, hahahahah
Duh sasa ANANYONGWA sijui km atampakata tena
yaani mm isingesimama wima, lkn huko Butimba aoe au aolewe tu
Mwanza nakuja
 
Back
Top Bottom