Mwanza: Mradi wa maji chazo cha Ziwa Victoria Butimba Mwanza kazi imekamilika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Your browser is not able to display this video.
Ikumbukwe kwamba Tarehe 14 mwezi October 2024 katika Maadhimisho ya Kilele cha Mwenge wa Uhuru Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumzia hali ya huduma ya Maji Mwanza aliweka bayana kuwa mwezi huu wa Octoba mradi mkubwa wa Maji wa chanzo cha Ziwa Victoria utakamilika.

Mashuhuda wamefika na wamejihakikisha hakika kweli kazi imekamilika kama Mhe Rais alivyowajulisha wana Mwanza na wanatuma salam za shukrani kwa Mhe Rais na kumpa ripoti ya kazi.

Jambo kubwa na shauku ni kumsubiri Mhe Rais kuja kuzindua rasmi Mradi huu muhimu sana kwa wana Mwanza na viunga vyake.

Kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huu kutaongeza upatikanaji wa maji Jijini Mwanza kutoka lita milioni 90 kwa siku za sasa hadi kufikia lita milioni 138 kwa siku.

Mradi huu utanufaisha Wakazi wa maeneo ya Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Nyamazobe, Nyahingi, Buganda, Luchelele, Lwanhima, Sahwa, Fumagila, Kishiri na Igoma kwa upande wa Jiji la Mwanza wakati kwa upande wa Magu ni Kisesa, Bujora na Isangijo.

Pia, soma:
√ - Mwanza: Mradi wa maji chazo cha Ziwa Victoria Butimba Mwanza kazi imekamilika

KERO - √ - Tatizo sugu la Maji jijini Mwanza

KERO - √ - Changamoto ya upatikanaji maji kata ya Buhongwa Mwanza-Nyamagana

KERO - Mwanza, ukosefu wa maji ni shida kubwa ya muda mrefu

Ni aibu Jiji la Mwanza siku 7 bila maji na Ziwa Victoria bado halijakauka
 
Hivi vyeo vya Dkt sijui Professor kuna siku mkesha wa kusoma bajeti kuu mwaka huu wa fedha Dkt Rioba wa TBC alifanya live covarage ya kuchambua bajeti yetu wazungumzaji mezaa kuu walikuwa ni Dkt na professor wa Chuo Cha Mipango IRDP Dodoma yani nilitafta concept yawanacho kizungumza nikaunganisha wale ndio wakufunzi wa Mipango ya Nchi ni ka conclude Kama walimu wako vile sijui wanafunzi watakuwaje? Tittle kubwa za elimu ila kichwani weupe.
 
Kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huu kutaongeza upatikanaji wa maji Jijini Mwanza kutoka lita milioni 90 kwa siku za sasa hadi kufikia lita milioni 138 kwa siku.
Hongera sana wahusika kukamilisha Mradi huo. Maji ni muhimu Sana katika Jamii.

Changamoto ya Maji maeneo tajwa yanakuzwa sana na leakage ya Maji hayo kwenye mitaa!!
===
Sina hakika kama Wana hakiki kiasi cha Maji kinachogawiwa (supplied) kwa wateja kutoka kwenye chanzo ndicho mita za Maji kwa wateja zina rekodi na kulipiwa. Kama hesabu hizi hazifanyiki za kujua kilichotumwa kwa wateja ndicho wateja wamepata... Uendeshaji wa Mamlaka za Maji utakuwa mgumu na tija itakuwa ngumu kupatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…