Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mashuhuda wamefika na wamejihakikisha hakika kweli kazi imekamilika kama Mhe Rais alivyowajulisha wana Mwanza na wanatuma salam za shukrani kwa Mhe Rais na kumpa ripoti ya kazi.
Jambo kubwa na shauku ni kumsubiri Mhe Rais kuja kuzindua rasmi Mradi huu muhimu sana kwa wana Mwanza na viunga vyake.
Kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huu kutaongeza upatikanaji wa maji Jijini Mwanza kutoka lita milioni 90 kwa siku za sasa hadi kufikia lita milioni 138 kwa siku.
Mradi huu utanufaisha Wakazi wa maeneo ya Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Nyamazobe, Nyahingi, Buganda, Luchelele, Lwanhima, Sahwa, Fumagila, Kishiri na Igoma kwa upande wa Jiji la Mwanza wakati kwa upande wa Magu ni Kisesa, Bujora na Isangijo.
Pia, soma:
√ - Mwanza: Mradi wa maji chazo cha Ziwa Victoria Butimba Mwanza kazi imekamilika
KERO - √ - Tatizo sugu la Maji jijini Mwanza
KERO - √ - Changamoto ya upatikanaji maji kata ya Buhongwa Mwanza-Nyamagana
KERO - Mwanza, ukosefu wa maji ni shida kubwa ya muda mrefu
Ni aibu Jiji la Mwanza siku 7 bila maji na Ziwa Victoria bado halijakauka