Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kanami, Kijiji cha Isangijo wilayani Magu Mkoani Mwanza Robert Mfungo anatuhumiwa kumbaka shemeji yake ambae ni mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka kumi na mbili.
Inaelezwa Mke ambaye ni Dada wa Mtoto huyo pamoja na majirani waligundua Unyama huo na kuamua kukaa kimya
CloudsDigitalUpdates
----
Inaelezwa Mke ambaye ni Dada wa Mtoto huyo pamoja na majirani waligundua Unyama huo na kuamua kukaa kimya
CloudsDigitalUpdates
----
Mbakaji huyo kwa muda mrefu amekuwa akiwabaka watoto wadogo wenye umri wa miaka 10-12 lakini amekuwa akishindwa kuchukuliwa hatua kutokana na nguvu ya mkuu huyo wa wilaya.
Tukio la hivi karibuni ambalo lilitokea Agousti mosi katika kitongoji cha Kinami ni la mtoto mwenye umri wa miaka 12 kubakwa na ROBERT MFUNGO.
Inaelezwa kywa, mbakaji huyo, anafanya vitendo hivyo kutokana na KALII kumkingia kifua pindi anapofikishwa kwenye vyombo vya dola.
Tukio hilo lililofanyika Agousti mosi ni la mwanafunzi anayesoma shule ya msingi ya Igekemaja iliyopo kata ya kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza.
Taarifa zinaeleza kuwa, KALII anamkingia kifua mbakaji huyo kutokana vijisenti na mashamba anayopewa na rafiki yake.
Miongoni mwa mashamba aliyopewa ni ambalo lipo Kijiji cha Isangijo ambalo lilikuwa ni mali ya mbakaji huyo ROBERT na sasa ni mali ya mkuu huyo wa wilaya.
Mkuu huyo wa wilaya anamtetea mtuhumiwa huyo wa ubakaji ambaye mara kwa mara katika mkutano wa kijiji umekkuwa akiazimiwa kuondolewa kijijini hapo.
Hata hivyo, mara baada ya mkutano wa kijiji kuazimia kuondolewa kwenye uongozi na kufukuzwa kwenye Kijiji hicho, mkuu huyo amekuwa akiendelea kumkingia kifua kwa kutengua maazimio ya wanakijiji.
Tukio la Agousti mosi ni la pili kwa mbakaji huyo wa watoto kwenye Kijiji hicho na anatumia nguvu ya fedha kudhalilisha watoto.
Tayari Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mtuhumiwa mbakaji huyo ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Kanami kilichopo Kijiji Cha Isangijo wilayani Magu, ROBERT MFUNGO.
MFUNGO amekamatwa kwa kubaka mtoto mwenye umri wa miaka 12 anayesoma darasa la sita shule ya msingi Igekemaja kata ya Kisesa wilayani humo.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Ramadhan Ng'anzi amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kwamba anashikiliwa katika kituo kikuu cha Polisi wilaya ya Magu mkoani humo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Isangijo, Malimi Pombe amenukuliwa akieleza kuwa Mtuhumiwa huyo sio mara ya kwanza kufanya vitendo hivyo.
Tukio hlo limeyaibua mashirika ya kutetea haki za wasichana na wanawake likiwemo shirika la kivulini chini ya Mkurugenzi wake YASSIN ALLY ambaye ameliomba Jeshi la Polisi kuacha kufumbia macho watu wanaojihusisha na vitendo hivyo. na kueleza kuwa kitendo hicho sio cha kufumbiwa macho.
Mkurugenzi huyo amewataka na wananchi kuendelea kuibua matukio hayo ya kijinsia ili pale wale wote wanaobainika waweze kuchukuliwa hatua.
Matukio ya udhalilishaji wa kijinsia yanatajwa kuongezeka katika mkoa wa mwanza huku wengi wa wanaodaiwa kufanya vitendo hivyo ni ndugu wa karibu.