Mwanza: Polisi wawaambia Bodaboda "acheni kudanganya wanafunzi kwa chipsi"

Mwanza: Polisi wawaambia Bodaboda "acheni kudanganya wanafunzi kwa chipsi"

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Kanda ya Mjini Kati, Ramadhan Jacobo amewaasa waendesha pikipiki wenzake kujiepusha na tabia ya kutongoza pamoja na kujihusisha na mapenzi na wateja wao.

“Asilimia tisini ya abiria tunaowabeba na wanaotulipa fedha ni wadada, na nyie ni mashahidi ukimpata na kumtongoza tu huyo umempoteza na akikubali umeanza kula hasara,” alisema Jacob.

Ameyasema hayo wakati waendesha pikipiki Mkoani Mwanza wakati wa kampeni ya kuzuia na kutokomeza watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu leo Aprili 13, 2022.

Naye, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Kata ya Mirongo Fatuma Mpinga aliwaasa waendesha pikipiki kuzingatia sheria za usalama barabara ili kuepusha ajali zinazoepukika.

"Natambua mnafahamiana na watu wengi sana wema na wahalifu, niombe muwafichue wahalifu maanake sisi sote tunahitaji usalama. Pia tunzeni familia zenu acheni kudanganya wanafunzi kwa chipsi huku nyumbani mnaacha elfu mbili halafu unarudi nyumbani unakuta kuku na unakula bila aibu,” aliongeza Fatuma.

3 (5).JPG

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kata ya Mirongo, Fatuma Mpinga
Akizungumza katika tukio hilo Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto la KIVULINI, Yassin Ally alisema bodaboda wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya uhalifu ikiwemo tabia ya kushawishi wanafunzi na kujihusisha nao kimapenzi.

“Ukilinganisha sababu za watoto kuwepo ama kutowepo mtaani unakuta hasara za kuwepo kwao mtaani ni nyingi mno kuliko faida, hivyo hatuna budi kama jamii mkiwemo waendesha bodaboda na makundi yote yakiwemo ya wanawake wajasiriamali, viongozi wa dini na kila mmoja wetu kushiriki kikamilifu ili kufanikisha kampeni ya kuondoa watoto mtaani itakayodumu kwa muda wa wiki nane,” alisema Yassin na kuongeza:

“Waendesha bodaboda mfanye kazi hii kwa faida ya familia zenu, mkumbuke kuwa ngono na ulevi hazijawahi kubadilisha maisha ya mtu, hivyo acheni kuweka heshima baa bali wekeni heshima majumbani mwenu.”

Aiadha, baadhi ya waendesha pikipiki wakizungumza katika mkutano huo walikiri wengi wao kuwa na tabia ya kuwarubuni wanafunzi pamoja na kutembea na wake za watu huku wakidai baadhi yao wamekuwa wakifanya hivyo kwa kushawishiwa.

"Watoto wengi wa mtaani wanatokana na sisi waendesha bodaboda kutokana na wengi wengi kuwa na tabia ya kuzaa na kisha kutelekeza,ni lazima tuambiane ukweli kama tukitaka kutibu tatizo hili,” alisema Francis John mmoja wa waendesha pikipiki katika Kata ya Mirongo.



Source: Malunde
 
Tusi kubwa sana kawaambia na kama wanajielewa watajirekebisha wenye tabia za kuacha Buku 2 na akirudi akakuta Kuku anakula bila aiba
Kweli hilo ni dongo
 
kampeni ya kuzuia na kutokomeza watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu leo Aprili 13, 2022.
Watawaua wote kwa kuwadondosha kwenye pikipiki au watawatokomezaje
 
Back
Top Bottom