Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan yuko katika siku ya 2 ya ziara yake Jijini mwanza ambapo leo tarehe 14 Juni, 2021 atakagua Mradi wa Ujenzi wa Daraja la JPM (Kigongo -Busisi), utafungua Mradi wa Maji Misungwi na kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) (Mwanza - Isaka).
Tutapeana update hapa kwa kila kilachojiri.
Karibuni.
====
UPDATES:
=====
Rais Samia asimamishwa na wananchi njiani mkoani Mkuyuni, Butimba mkoni Mwanza
Wananchi wasema kuwa maeneo ya pembezoni hayana umeme wa kutosha, Rais Samia asema kuna mradi unaitwa mradi wa ujazilizi ambao utakuja kujaliza umeme katika maeneo hayo na pia akassema kama wananchi walivyosikia kwenye bajeti kuwa ghrama ya kuweka umeme imepunguzwa kutoka 350,000 hadi shilingi 27,000. Asema umeme utumike kwa mambo ya kiuchumi ili unifaishe maisha ya watu kama saluni welding nk.
Pia asema kuna kulipa fidia kwa maeneo ambayo Halmashauri ilichukua kwa wananchi na halmashauri imeshalipa bilioni 4 zilizobaki wanazitenga waje kumaliza kulipa fidia.
Kwa habari ya wodi ya wanaume Butimba adai Akitoka yeye Mwanza Makamo wa Rais atakwenda Mwanza kuifungua Wodi hiyo. Na pia kazi iendelee wanawake kwa wanaume wafanye kazi ili kijenga Taifsa uchumi uende mbele. Pia aliambiwa watoto wanakaa chini, amesema hiyo ni kazi ya halmashauri watawakamata halmashauri ili waweze kupeleka madawati.
Pia Rais Samia achangia mfuko wa ujenzi wa CCM Butimba kiasi cha shilingi milioni 5 ili waweze kukamilisha ujenzi wao. Amefanya hivyo baada ya wanachi ambo pia ni wanachama wa Chama cha CCM Butimba kumuomba kufanya hivyo.
Mbunge wa Butimba
Mh. Rais tunakukushuru na tunakupenda sana na kwa kusimama hapa kata ya Mkuyuni na Butimba na pia tunashuru kwa kupokea sh milioni 500 kwa ajili ya kuboresha hospitali yetu ya wilaya ambayo ilikuwa haikiddhi mahitaji sawasawa. Tunakurukuru kwa barabara ya Buhongwa kutoka Mkuyuni kwenda mpaka Kanyerere Tambuka reli kwenda mpaka Madina kuna barabara nyingine ya KM 11 na ipo kwenye mpango wa TAKTIKI na sisi tutaipisha kwa kishindo ili barabara hii ije ijengwe. Pia tunahitaji huu mpango wa maji mwakani ukamilike ili wananchi wapate maji.
Rais Samia asimamishwa Buhongwa Mwanza
Rais aomba viongozi wa dini kufanya maombi na Dua kabla ya kuendelea kuongea na wananchi.
Waziri wa Ummy Mwalimu
Asema kuwa alikwenda Mwanza aliagizwa apeleke kiasi cha sh milioni 300 kwa ajili ya kituo cha afya cha Buhongwa hilo tayari ameshaelekezwa na atapeleka hizo fedha kwa ajili ya wodi ya kujifungulia kina mama na mambo mengine.
Pia bajeti imebainisha mradi mkubwa ambao itaenda utaenda kuboresha barabara za miji vijiji pamoja na halmashauri ya jiji la Mwanza na swala la madawati pamoja na vyoo vya wanafunzi wanalifanyia kazi.
Rais Samia Suluhu Hassani Buhongwa
Swala la mradi wa maji tayari unaendelea na zile lita alizozisema mbunge na zile zilizopo wanakwenda kufikia asilimia 85. Na swala lingine ni ucheleweshaji wa mikopo na hilo halamashauri wanalifanyia kazi, na sio mikopo hiyo itolewe kwa vikundi vile tu ambavyo wanaweza kweli kuzifanyia kazi na si kila kikundi kipewe tu ili mradi kila kikundi kimepata.
Rais Samia asimama Kigongo
Eng. Patric Mfugale Atoa taarifa ya Mradi wa Daraja la JPM kOGONGO Busisis asema kuwa, daraja hilo ni kubwa awali lilikuwa linaitwa daraja la Kigongo Busisi ila sasa linaitwa Daraja la JPM ni daraja lenye urefu wa mita 3200 la sita kwa ukubwa Afrika. Daraja hili lilijengwa kuwa ili uvuke pale ilikuwa ni lazima utumie vivuko 2 na ilikuwa inatumika hadi saa2 hivyo kuchelewesha shughuli za kiuchumi.
Rais Samia apita kukagua daraja la Magufuli hiyo ni baada ya kupewa maelezo na Eng Mfugale juu ya ujenzi huo, kisha ataelekea wilayani Misungwi kwenda kuzindua mradi wa maji. Kwa mujibu wa Msimamizi wa mradi wa daraja la Magufuli, daraja hilo litakamili 2023. Na ukamilikaji wa daraja hilo litafungua muingiliano wa mikoa ya Kagera na Kigoma.
Mbunge wa Sengerema, TabasamAsema rais ametoa leseni ya mradi wa dhaahabu ambayo ilikuwa imegoma kutoka kwa muda wa miaka minne pia amesema pale Sengerema wana vyuo 3 vya VETA ila havina vifaa, hivyo anamuomba Rais apeleke vifaa ili wananchi wapete elimu katika vyuo hivyo ili waweze kufanya kazi katika migodi. Tunayo miradi mikubwa ya maji tunaomba mhe, Uweso arudi kuja kuangalia mradi mkandarasi hajaonekana kwenye mradi kwa muda na pia wilaya ya Sengerema wanakatiwa maji hawajui tatizo ni nini, pia wana ujenzi wa sekondari 15 baada ya kuruhusu elimu bure wanajenga shule za sekondari hivyo wanahitaji msaada wa serikali katika kuezeka shule hizo.
Mbunge wa Buchosha, Shigongo
Hospitali ya wilaya ilikamiliaka mwaka 2017 ila hakuna madawa, pia barabara ya kutoka Sengerema uliahidi kutengeneza barabara hiyo naomba angalau hata KM 10 za kuanzia zitengenezwe.
Rais Samia Suluhu Hasani akiwa Sengerema Kwanza niwapongeze kwa mgodi wa Nyanzaga kupata kibali na wanasengerema mtakwenda kupata kazi pale na pia ile hisani itakayotolewa itatatua shida ndogondogo kama maji, madawati umeme nk pia Sengerema hamko vizuri kwenye matumizi ya fedha, halmashauri ya Sengerema haikusanyi pesa za kutosha lakini pia inafuja pesa zinazoletwa hivyo serikali tumeleta wakaguzi maalumu waje kufanya ukaguzi.
Lakini nizungumzie swala la kituo cha afya najua kuna uhaba wa madawati watumishi lakini hivi punde tumetoa tangazo la ajira kwa waalimu na watumishi wengine na watumishi hawa tutakapo waajiri tutawasambaza nchi nzima na watakuja mpaka huku Sengerema.
Lakini inashangaza kusikia hapa Sengerema kuna deni mnadaiwa serikali kuu tunajitahidi kuleta fedha ila unasikia deni na hospitali hakuna vifaa hapa inaonesha udhaifu wa uongozi, mara inadaiwa umeme sasa kama wananchi wanalipa bili kwa nini na wao washindwe kulipa bili.
Naambiwa wancnhi wanakosa maji kwa sababu shirika la maji linadaiwa bili za umeme sasa kama wananchi wanalipa bili za maji kwa nini wao wanashindwa kulipa bili za umeme hapa kunaonesha Sengerema inabidi iangaliwe.
Swala lingine ni swala la umeme naambiwa kasi ni ndogo lakini nataka kuwaahidi ifikapo 2024 Tanzania nzima pamoja na vijiji vyake itakuwa imepata umeme mijini na vijiji kwa sababu kazi kubwa inafanywa na wizaraya nishati kwa sababu sisi serikali tunajitahidi kwa ajili ya kutoa fedha kuwalipa wakandarasi na hiyo itakuwa imebaki kazi ya TANESCO kwa ajili ya kuunganisha umeme.
Lakini lingine ni tatizo la baraza la ardhi lakini Sengerema tumeshatoa kibali baraza liundwe, lingine ni tatizo la stand lakini serikali tumeshatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa standi. Na lingine ni Veta Sengerema tutakwenda kukaa na wizara husika tuone tutakavyoweza kufanya kusogeza vifaa ili vijana waweze kupata elimi.
Pia kuna swala la shule za sekondari, lakini mbunge wenu ameshaambiwa achugue eneo ili shule ziweze kujengwa na pia tunakwenda kujenga shule za sekondari na sekondari za wasichana tu ambazo zitakuwa za sayansi. Na mambo yote yanafanyiwa kazi. Lakini kila mradi unaoletwa kwenu naomba sana tunzeni kwa kuwa zile ni mali za wana sengerema. Pia mtunze amani na utulivu, kwa kuwa amani na utulivu unawapa utulivu serikali kuu ili waweze kuleta miradi zaidi badala ya kuhangaika kuleta utulivu ila Sengerema nawapongezammetulia.
Wananchi nawataka mkafanye kazi na kutimiza majukumu yenu, fanyeni kazi ili muweze kulipa kodi. Manapolipa kodi mnatupa uwezo wa kuleta miradi pia kuweza kurudisha pesa tulikopa, Miradi hii tunakopa fedha, fedha nyingi sana. Daraja hili mnaloliona mimi hesabu zake naziona tu kwenye makaratasi ni fedha nyingi mmo ni mabilioni mi saba ni pesa nyingi mno. Sasa ili tuweke kurejesha kule tulipokopa ni kwa nyinyi kufanya kazi na kuweza kulipa kodi, hivyo mlipe kodi kama mnavyopangiwa na halamashauri.
Uzinduzi wa mradi wa Maji Misungwi Mwanza
Rais Samia amewasili Misungwi na tayari yupo mbele ya Tenki la maji kwa ajili ya kulizindua. Maji yanamiminika katika bomba na tayari tayari tenke limezinduliwa baada ya kufungua kile kitambaa kilichofunika jiwe la msingi. Mhandisi wa mradi wa maji
Mradi wa maji una jumala ya gharama ya kiasi cha shilingi bilion 13.77 na umejengwa kupitia chanzo chake cha Ziwa Victoria, na unajengwa kupitia program ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira.
Juma Aweso, Waziri wa maji
Nina kazi moja tu ya kuja kumakribisha Rais Samia kama mnavyofahamu mwanamke yoyote hafundishwi kulea mtoto basi Mwanamke huyu Rais samia ni jembe. Nitumie nafasi hii kukushuru wew kwa kutuamini sisi viaongozi wa maji.
Nakumbuka mara baada ya uteuzi wangu uliniita ofisini ukanambia maneno machache ambayo leo nataka kuwaambia wananchi wa Misungwi, Alinambia kuwa kila tulikopita kuzunguuka kuomba kura kilio kikubwa kilikua ni maji na umesema sasa nguvu na mipango unataka kuona maji bombani kwa kuwa umeona wanawake wanavyoteseka kwa kutafuta maji .
Maji hayani mbadala maji si kama chakula kwamba ukikosa ugali utakula makande au ukikosa wali utakula ugali, maji ukikosa maji huna mbadala utapa magonjwa na adha kubwa. Nasi tunakuahidi kuwa tutasimia miradi wananchi wapate maji na si maji tu bali maji safi na salama.
Pia nataka kusema asitokee mtu akawa aanwabambikia wananchi bili za maji, unataka kuunganisha maji nyumbani kwako unapewa magharama ambayo hata haijulikani yanatoka wapi, mtu huyo hata awe na mapembe kamaa nini tutayakata na wananchi watapata maji.
Sisi Wizaraya maji tunaendelea kufanya mageuzi ili kuhakikisha wananchi wanaendeleea kupata maji na kumtua mama ndoo kichwani.
Rais Samia Suluhu Hassan azungumza
Eneo la umeme vijiji vyote 42 vilivyobaki katika vijiji tunakwenda kuvipa umeme na wakandarasi walishatafutwa na hapa nipo kuzindua mradi wa maji.
Niwashukuru wabia wa maendelo waliotusaidia katika kukamilisha mradi huu, hii itafanya watu wa Misungwi kupata maji kwa asilimia 100, na niwapongeze kwa kupata mradi huu mkubwa.
Pia najua sio wananchi wote wamesambaziwa maji japo mradi huu upo hapa hivyo nitoe wito kwa wizara na mainjinia kuwasambazia maji wananchi wote ili waweze kuyatumia.
Pia kuna miradi mingine inayoendelea Mwanza ambayo inaendelea katika maeneo kadhaa ikikamiliaka itatumia bilioni 30.8 lengo letu ni kutekeleza kikamilifu ilani ya uchaguzi. Lakini pia utekelezaji wa wa lengo la 6 la dunia kuleta maji safi.
Nitoe wito kwa wana Misungwi kulinda miundombinu ya maji ni gharama ni mabilioni mengi ukichukua yale mabilioni ukayagawanya kwenye gharama hakuna atakayeweza kuyanunua maji na ndio maana hakuna sekta binafsi inayofanya miradi hii kwa kuwa wao watataka kurudisha faida. Kwa hiyo kama serikali inatumia pesa za ndani au mikopo au misaada lakini inatumia ghrama kubwa ili kuleta maji hamna budi kuyatunza na kutunza mradi.
Kingine ni kutunza mazingira ikiwomo na vyanzo vya maji, naomba mrudi kuwa rafiki wa mazingira mtunze vyanzo vya maji. Leo hii tumetoa maji kwenye ziwa ziwa hili ni chanzo na ziwa hili linatiririsha maji sehemu nyingine sasa sio kwamba litakuwepo siku zote daima dumu ili lidumu lazima tulitunze na kulilinda.
Wito wangu mwingine kwenu kwa Misungwi na watu wote wa Mwanza lipeni bili za maji na pia MWAUSA msibambikie mtu bili mpenzi mtu bili kulingana na anavyotumia, mkibambikia mtu bili hawatalipa ila watatafuta jinzi ya kutumia maji bila bili.
Ziara ya Rais Samia Suluhu Fela, Mwanza kuzindua ujenzi wa reli
Ndugu zangu nianze kuungana na wote waliotangulia kumshukuru Mungu na wote tuko hapa kwenye tukio hili muhimu, Napenda kuwashukuru kwa kunialika na kama moja ya ahadi zetu ni kuendelea kutekeleza ujenzi wa reli hii na miradi iliyoasisiwa na hayati Magufuli hii ndio sababau nimefurahi kuwepo hapa kuweka jiwe la msingi la mradi wa reli yenye urefu wa km 341 na itakayogharimu kiasi cha sh Trilion 3.1.Nawashukuru wananchi mliojitokeza kwa wingi hii inaonesha mnatambua umuhimu wa mradi huu.
Ndugu wana Mwanza nchi yetu inatekeleza sera za uchumi wa viwanda katika sera hii tutahitaji njia bora ili kusafurisha mazao ya kilimo na migodi na viwanda. Reli hii tunayoijenga itarahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa na itashusha gharama za usafirishaji wa Bandari kwa watu wa ndani hadi nchi jirani kama mlivyoambiwa reli hii tutakwenda nayo hadi nchi jirani.
Lakini naomba mtambue kwamba moja ya mambo yanayokwamisha kasi ya ukuaji kiuchumi barani Afrika ni miondombinu duni na ukosefu wa miundombinu kabisa. Lakini ukosefu wa miundombinh bora na kutokuwepo kwa miundombinh kunakosesha uwepo wa huduma bora na kuchelewesha upatikanaji wa bidhaa na kufanya uwekezaji barani Afrika kuwa mdogo.
Leo tupo hapa kuweka jiwe la msingi na mradi huu tutakwenda nao hadi Kigoma na maeneo mengine na na tunaijenga kwa vipandevipande lakini niwahakikishie kuwa tutaijenga yote na kuikamilisha.
Faida zimetajwa nyingi na msanii wetu Barobaro ametaja baadhi nami nitazigusia baadhi.
- Mradi unatarajiwa kutengeneza ajira 11 elfu
- Reli itapunguza muda wa kusafiri kutoka masaa 17 ya mwanzo mapa masaa 8 kutoka Mwanza Mpaka Dar es Salaam kwa mabasi na treni. Pia itapunguza gharama za usafirishaji na kuongoza upatikanaji wa mapayo.
- Pia reli itakuwa na uwezo wa kusafirisha tani nyingi na kusaidia kulonda barabara, mizigo imekuwa ikisafirishwa na mabasi na kusababisha uharibifu wa barabara hasa kwa sababu baadhi ya madereva kutozingatia viwango vya uzito na kwa ujenzi wa reli hii tutalinda barabara na hivyo barabara zetu zitadumu muda mrefu.
- Tano reli hii itasaidia kuchochea shughuli zingine za kiuchumi kama viwanda kilimo na utalii kuna watalii watapanda reli hii.
Pia kwa kuwa reli hii ni ya kanda ya ziwa basi kutakuwa na mabehewa maalumu kwa ajili ya kubebea samaki na nyama na hivyo kuwanufaisha wavuvi na wafugaji.
Kuna jambo ambalo mwenyekiti wa kamati ya ujenzi aliniomba kuhusu ununuzi wa vichwa vya treni na tayari waziri aloshalijibu nimiuwa kufikia Decemba mwaka huu tayari tutakuwa tumenunua na stock ya pili itakuja mwaka ujao lakini stock ya kwanza ya majaribio itakuwa tayari ipo mokononi.
Reli inayojengwa itakuwa inatumia umeme hii ndio sababu tunaendelea na ujenzi wa bwawa la Mwl Nyerere utakaogharimu trilion 6.5 utakaozaliza umeme Mgh 2115 na mpaka sasa umefikia asilimia 51.2 na tunaendelea na ujenzi wa miondombinu Mwanza na kabla sijaja hapa nimetoka kukagua mradi wa ujenzi wa Daraja Busisi na tunaendelea na ujenzi wa barabara.
Na kila miradi inayotekelezwa inakuja na fursa ya ajira na biashara hivyo wana Mwanza changamkieni fursa.
Miradi inayokuja inatumia gharama kubwa sana hivyo nawasihi wana Mwanza na watanzania kwa Ujumla kuendelea kulipa kodi mnapolipa kodi mnatupa urahisi wa kutekeleza miradi msipolipa kwa wakati tunakuwa tunasuasua. Mfano hapa tunahitajj kutekeleza mradi wa ukarabatk wa hospitali ya wilaya.
Baada ya hotuba Rais Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa reli.