Mwanza: Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) umefikia 96.3%

Mwanza: Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) umefikia 96.3%

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Katika juhudi za kuimarisha miundombinu na kukuza uchumi wa Taifa, ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) umeendelea kuwa kielelezo cha mafanikio makubwa chini ya uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Abdallah Ulega akiwa ziarani katika Mkoa wa Mwanza na alipotembelea daraja hilo Januari 24, 2025 amesema, daraja hilo, ambalo linatarajiwa kuwa refu zaidi Afrika Mashariki, ni mfano bora wa utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), likilenga kuunganisha mikoa ya Mwanza na Geita huku likirahisisha shughuli za kijamii, kiuchumi na kibiashara kwa mamilioni ya Watanzania.

"Kwa juhudi za dhati za Rais Samia, mradi huu uliokutwa ukiwa asilimia 25 mwaka 2021, sasa umefikia zaidi ya asilimia 96.3 ambapo uwekezaji wake wa shilingi bilioni 611 unaonesha dhamira thabiti ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha Watanzania wanapata maendeleo ya haraka na endelevu." alisema Waziri Ulega na kuongeza

" Kukamilika kwa daraja hili lenye urefu wa kilomita 3 na barabara unganishi za kilomita 1.6 kutapunguza muda wa kuvuka kutoka masaa mawili hadi dakika 5 tu."

Pia, soma: Moja kati ya miradi ya kimkakati nchini Tanzania ni pamoja na mradi wa Daraja la Magufuli almaarufu daraja la Kigongo Busisi linalopita juu ya ziwa

Daraja hili ni kielelezo cha mapinduzi makubwa ambayo yataongeza kasi ya uchumi kupitia usafirishaji wa bidhaa na huduma kati ya mikoa na nchi jirani kama Uganda, Rwanda na Burundi.

Aidha, daraja hili limesanifiwa kwa viwango vya kimataifa na litadumu kwa zaidi ya miaka 100, likiwa ni hazina kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella amepongeza kazi kubwa anayoifanya, Rais Dkt. Samia kuhakikisha miundombinu ya kisasa inajengwa kwa kasi na kwa viwango vya hali ya juu.

"Sisi Geita itakua zaidi na shughuli za kiuchumi zitakua zaidi na zitachochewa kwa kiwango kikubwa na daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) pale litakapokamilika" alisema Shigella na kusisitiza

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Michael Lushinge ameeleza utekelezaji wa mradi huo kama ishara ya kielelezo cha kauli mbia ya Rais ya Kazi Iendelee

"Mheshimiwa Rais Samia, ahadi yako ya kuhakikisha kazi inaendelea imeonesha matokeo makubwa kupitia mradi huu. Watu wa Mwanza, Geita na kanda nzima ya Ziwa Victoria wanakushukuru kwa maono yako ya kipekee." alisema Lushinge na kuongeza

"Wakati Rais Samia anaingia madarakani, nguzo za daraja zilikuwa bado ziko kwenye maji lakini leo nguzo ziko juu na magari yanaweza kupita. Hii inaonesha falsafa yake ya Kazi Iendelee ni kweli na tunaona kazi imeendelea."

Ni dhahiri kuwa daraja hili si tu linarahisisha usafiri, bali linatoa nafasi ya ukuaji wa uchumi wa wakulima, wavuvi, wafugaji, wachimbaji wa madini na sekta zingine muhimu."


ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) ni ushuhuda wa maono makubwa na uongozi imara wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Alipoingia madarakani, mradi huu ulikuwa umefikia asilimia 25 tu, lakini chini ya usimamizi wake thabiti, sasa umefikia zaidi ya asilimia 96.3, ukiwa hatua chache tu kuelekea kukamilika. Hili pia ni kielelezo cha dhamira yake ya kuendeleza miradi mikubwa kwa maslahi ya Taifa.
IMG-20250124-WA0100.jpg
IMG-20250124-WA0101.jpg
IMG-20250124-WA0102.jpg
IMG-20250124-WA0103.jpg
IMG-20250124-WA0104.jpg
IMG-20250124-WA0106.jpg
IMG-20250124-WA0107.jpg
IMG-20250124-WA0105.jpg
IMG-20250124-WA0108.jpg
IMG-20250124-WA0109.jpg
 
Back
Top Bottom