Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Ni patashika. Ndivyo unavyoweza kuelezea mvutano kati ya wafanyabiashara wadogo jijini Mwanza na mamlaka ya Jiji hilo baada ya wafanyabiashara hao kuandamana leo Jumamosi Oktoba 23,2021 na kufunga barabara ya Nyerere eneo ya Voil kushinikiza kupewa vizimba kwenye maeneo rasmi.
Kundi la wafanyabiashara hao lilijumuisha walioondolewa katika mtaa wa Makoroboi na kuhamishiwa katika soko la Mchafu Kuoga na maeneo mengine ambayo ni rasmi kufanya biashara zao.
Athuman Makelele, aliyekuwa katika soko la Makoroboi ni miongoni mwa wafanyabiashara walioshiriki maandamano hayo huku akidai wamelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya juhudi za kushinikiza viongozi wa Jiji kuwapangia maeneo yanayowatosha kugonga mwamba.
"Tumefika hapa asubuhi hakuna muafaka wowote kutoka kwa viongozi, tunapiga simu wamezima tukaona sasa tuzibe barabara ili waje watusikilize ikibidi watupangie maeneo yanatosheleza idadi yetu kama machinga," amesema Makelele
Naye Khalfan Mohammed amesema soko la Mchafu Kuoga ni finyu ikilinganishwa na idadi ya wafanyabiashara waliyoondolewa katika soko la Makoroboi.
"Hawa waliowahi wakapewa meza hapa sio waliyokuwa Makoroboi, sasa sisi tuliokuwa kule mjini tukaambiwa tuje hapa tumefika tukakuta watu wameshagawana maeneo yameisha," amesema Khalfan.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amesema amepokea malalamiko ya wafanyabiashara hao huku akiwataka kujiorodhesha majina yao kwa viongozi wao kwa ajili ya kupewa vizimba katika maeneo mengine.
"Ombi lenu limepokelewa , tutalifanyia kazi na kuwaletea majibu kupitia uongozi wenu, ninachowaomba andikeni majina kwa viongozi wenu ili tuweze kuwapangia maeneo rasmi," amesema Makilagi
Chanzo: Mwananchi