BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wanafunzi hao ni kati ya 130 walioanza kidato cha kwanza mwaka 2019 kutoka Shule ya Sekondari Kishinda wilayani Sengerema ambao wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu hizo.
Baada ya kupokea taarifa ya shule wakati wa Mahafali, Diwani wa Kishinda, Shokolo Vicent ametoa maagizo kwa uongozi wa shule hiyo kulichukua jambo hilo kama la dharura ili kutokomeza vitendo hivyo.
Amesema “Haiwezekani wanafunzi 70 kushindwa kuhitimu kidato cha 4, hii ni aibu kwa shule na wazazi kwa ujumla, jambo hili halijanifurahisha kabisa. Lazima tutazame upya hili jambo kama kunashida mahali lazima tuitatue".
===================
Wanafunzi 70 wa Shule ya Sekondari, Kishinda, wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza watashindwa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2022 kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo mimba na utoro. Wanafunzi hao ni kati ya 130 walioanza kidato cha kwanza mwaka 2019. Kwa ujumla, shule hiyo ina wanafunzi 280, wavulana 147 na wasichana 133 huku walimu wakiwa 14.
Akisoma lisala ya shule hiyo kwenye maafali ya 14 ya shule hiyo leo Ijumaa, Oktoba 14, 2022, mwanafunzi wa shule hiyo, Paul Paskari amesema hali hii inadidimiza maendeleo ya shule hivyo jamii kwa kushirikiana na walimu inapaswa kukomesha hali wanafunzi waweze kufikia malengo yako.
Diwani wa Kishinda, Shokolo Vicent amekwerwa na hali hiyo na kuutaka uongozi wa shule hiyo kuchukuwa jambo hilo kama la dharura ili kutokomeza vitendo hivyo.
“Haiwezekani wanafunzi 70 kushindwa kuhitimu kidato cha nne hii ni aibu kwa shule na wazazi kwa ujumla,” amesema Vicent "Jambo hili halijanifurahisha kabisa, lazima tutazame upya jambo kama kunashida yoyote lazima tuitatue kwani inanisikisha sana,” amesema
Shokolo amesema Serikali inajitahidi kuboresha miundombinu ya shule zote nchi ili wanafunzi waweze kusoma lakini inashangazwa na hali hii uongozi wa shule unatakiwa kujitathimini.
Mkuu wa shule ya Sekondari Kishinda, Anton Bulugu amesema ana muda mfupi tangu alipohamia shuleni hapo hivyo hali hiyo atajitahidi kupambana na kuitomekeza. Amewataka wazazi kushirikiana na walimu ili jambo hilo kukomeshwa ili wanaoanza kidato cha kwanza wahakikishe wanamaliza.
Mkuu huyo wa shule amesema kwa tahimini ya matokeo ya shule hiyo kwa miaka mitatu inaonesha ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 82 hadi 95.
MWANANCHI