Mwanza: Wanafunzi 70 kati 130 wakwama kumaliza kidato cha 4 kisa mimba za utotoni

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wanafunzi hao ni kati ya 130 walioanza kidato cha kwanza mwaka 2019 kutoka Shule ya Sekondari Kishinda wilayani Sengerema ambao wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu hizo.

Baada ya kupokea taarifa ya shule wakati wa Mahafali, Diwani wa Kishinda, Shokolo Vicent ametoa maagizo kwa uongozi wa shule hiyo kulichukua jambo hilo kama la dharura ili kutokomeza vitendo hivyo.

Amesema “Haiwezekani wanafunzi 70 kushindwa kuhitimu kidato cha 4, hii ni aibu kwa shule na wazazi kwa ujumla, jambo hili halijanifurahisha kabisa. Lazima tutazame upya hili jambo kama kunashida mahali lazima tuitatue".

===================

Wanafunzi 70 wa Shule ya Sekondari, Kishinda, wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza watashindwa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2022 kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo mimba na utoro. Wanafunzi hao ni kati ya 130 walioanza kidato cha kwanza mwaka 2019. Kwa ujumla, shule hiyo ina wanafunzi 280, wavulana 147 na wasichana 133 huku walimu wakiwa 14.

Akisoma lisala ya shule hiyo kwenye maafali ya 14 ya shule hiyo leo Ijumaa, Oktoba 14, 2022, mwanafunzi wa shule hiyo, Paul Paskari amesema hali hii inadidimiza maendeleo ya shule hivyo jamii kwa kushirikiana na walimu inapaswa kukomesha hali wanafunzi waweze kufikia malengo yako.

Diwani wa Kishinda, Shokolo Vicent amekwerwa na hali hiyo na kuutaka uongozi wa shule hiyo kuchukuwa jambo hilo kama la dharura ili kutokomeza vitendo hivyo.

“Haiwezekani wanafunzi 70 kushindwa kuhitimu kidato cha nne hii ni aibu kwa shule na wazazi kwa ujumla,” amesema Vicent "Jambo hili halijanifurahisha kabisa, lazima tutazame upya jambo kama kunashida yoyote lazima tuitatue kwani inanisikisha sana,” amesema

Shokolo amesema Serikali inajitahidi kuboresha miundombinu ya shule zote nchi ili wanafunzi waweze kusoma lakini inashangazwa na hali hii uongozi wa shule unatakiwa kujitathimini.

Mkuu wa shule ya Sekondari Kishinda, Anton Bulugu amesema ana muda mfupi tangu alipohamia shuleni hapo hivyo hali hiyo atajitahidi kupambana na kuitomekeza. Amewataka wazazi kushirikiana na walimu ili jambo hilo kukomeshwa ili wanaoanza kidato cha kwanza wahakikishe wanamaliza.

Mkuu huyo wa shule amesema kwa tahimini ya matokeo ya shule hiyo kwa miaka mitatu inaonesha ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 82 hadi 95.

MWANANCHI
 
Watoto wa siku hizi wanapenda sana pipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shule za kata zina changamoto nyingi sana. Ukifuatilia kwa karibu kwenye hiyo shule, utakuta kugundua hakuna mabweni, huku watoto wakiishi/wakipanga kwenye mageto nje kidogo na shule ilipo!

Hivyo ukichanganya na umaskini wa familia zao, wanajikuta wamenasa kwenye vishawishi vya watu wabaya.
 
Najiuliza hapa Je hao 60 walio salia je wote ni boyz ?
 
Hili tatzo la mimba ni tatizo kubwa sana,niliwah kushangaa shule moja ya kata na ipo mjini lakini kila wakipima mimba sio chini ya wasichana kumi na tano walikuwa wanarudishwa nyumban na bado wengine walikuwa wakigundua wana mimba wanaacha wenyew,hapo ndipo nilipoamini watu hawajaogopa kabisa hii adhabu iliyopo
 
Hawafungwi wanaofungwa wachache wenye wazazi wenye uchungu,wengi wanaishia kumalizana nyumbani TU!
 
Wasukuma na shule wapi na wapi?wao kuolewa,kukimbilia migodini ndo mambo Yao...
Bado unajidanganya hivo? Wasukuma nenda vyuoni huko utawakuta wa kutosha! Nenda A-level huko ukachukue sensa! Hapo ulipo hujaona daktari au mwalimu msukuma? Au unaropoka tu!
 
Bado unajidanganya hivo? Wasukuma nenda vyuoni huko utawakuta wa kutosha! Nenda A-level huko ukachukue sensa! Hapo ulipo hujaona daktari au mwalimu msukuma? Au unaropoka tu!
Idadi ya wanaosoma na wasiosoma ndo inaongea kaka[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]!!!siropoki naongea facts,mfano si hukoo sengerema wanafunzi 130 wameacha shule !!!
Wasukuma ndo zaoo naongea uhalisia uliopo wasukuma wengi haswaa wanawake hawasomi
 
Wewe takwimu umepeta wapi? Mambo yamebadilika sana! Wewe ni kabila gani ambalo watu wenu wote wamesoma?
 
Kuchapiwa inauma sana nyii acheni tu. Mimi niligongewa demu karibu nijiue sasa ije iwe mke? Achaneni tu na ule mgodi unaotembea.

Masanja ni wa kuombewa na kupewa canseling.

mpwayungu village UMUGHAKA
 
Hivi ukimuona mwanao kakua kashabalehe , kwani si Kuna vijiti hata vya miaka mitano? Kwa Nini usimuwekee hicho kijiti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…