KERO Mwanza: Wananchi Nyegezi, Mkolani na Buhongwa kuna uhaba wa maji zaidi ya wiki nne. Hakuna taarifa rasmi kutoka mamlaka

KERO Mwanza: Wananchi Nyegezi, Mkolani na Buhongwa kuna uhaba wa maji zaidi ya wiki nne. Hakuna taarifa rasmi kutoka mamlaka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa zaidi ya wiki tatu hadi nne, wakazi wa maeneo ya Nyegezi, Mkolani, na Buhongwa jijini Mwanza wamekumbwa na uhaba mkubwa wa maji, bila taarifa yoyote rasmi kutoka Idara ya Maji.

Hali ni mbaya—wananchi wanalazimika kuchota maji kwenye mito na maji tiririka, ambayo ni hatari kwa afya na yanahatarisha maisha kwa magonjwa kama kuhara, kipindupindu na maambukizi mengine.

Cha kusikitisha zaidi, maeneo ya wakubwa bado yana maji, huku wananchi wa kawaida wakiteseka. Je, huu ni ubaguzi wa huduma? Au kuna hujuma dhidi ya juhudi za Mheshimiwa Rais ambaye alizindua mradi mkubwa wa maji hivi karibuni?

WITO:​

Tunatoa wito kwa Waziri wa Maji:

  • Vunja uongozi wa Mamlaka ya Maji Mwanza.
  • Tuma uchunguzi wa haraka.
  • Rejesha huduma ya maji kwa wananchi wote bila ubaguzi.
Maji ni haki ya kila Mtanzania – si anasa ya wachache.
 
Back
Top Bottom