Mwanza: Wananchi Wakesha kwenye ofisi za CHADEMA ili kuwahi Maandamano

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio Taarifa Mpya iliyotufikia usiku huu, kwamba Maelfu ya Wananchi wanamiminika kwenye ofisi zote chadema za Jiji hilo kwa lengo la kukesha ili kuwahi kujiandikisha, ili washiriki maandamano.

Wananchi wengi wanadhan kwamba i ili kushiriki Maandamano hayo ni lazima ujiandikishe, hivyo wamewahi kwenye ofisi hizo ili kujihakikishia namba za usajili.

Ukweli ni kwamba Maandamano ya Chadema hayana usajili , kila mtu aliyeguswa na ugumu wa maisha anashiriki tu.

Natoa wito kwa viongozi wa chadema Mwanza na kanda ya Victoria kuelimisha wananchi kuhusu jambo hilo.

 
Kawadanganye nyumbu wenzako huko!! Rubbish!!
 
hii iko low key sana dah 🤣

kinyonge zaid🐒

R I.P Laigwanan comrade ENL
 
Michango imekamilika?
 
Itakuwa waliona ule magawo wa posho za maandamano kutoka kwa Mnyika!
 
Lucas mwashambwa atatetemeka akisoma hii
 
CHADEMA ni wapuuzi sana!
Taifa liko katika majonzi na maombolezo ya Kitaifa ambayo yametangazwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dr.Samia Suluhu Hassan halafu wao wanakaidi na kuendelea kuandamana!

Musoma Mjini CHADEMA - Maandamano mmewambia viongozi wenu wapeleke waandamanaji 300 na wajigharamikie wenyewe vinginevyo viongozi wenu hao wawajibike!

CHADEMA - Maandamano inasema wao hawana hela.
Viongozi wenu ni kilio, wanasema nauli ya Tzs.24,000 (kwenda na kurudi Musoma - Mwanza) hapo bado Chakula wamesema wao hawana!

Ni propaganda tu hakuna Mwananchi mwenye akili timamu anaweza kukesha hapo CHADEMA kuwahi Maandamano! Labda hao ni vibaka wasiokuwa na mahali pa kulala!

Dr.Slaa naye mzuka umempanda baada ya Edward Lowassa kifariki anataka kuandamana/kusherehekea kifo cha Lowassa nanyi.

Maandamano yenu lazima yadode!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…