Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Watu 1,000 wamenusurika kifo baada ya stoo ya kuhifadhia mafuta ya petroli kulipuka na kuteketea kwa moto katika Kisiwa cha Benzi, Kata ya Kayenze, wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, ACF Elisa Mugisha, amesema tukio hilo limetokea Agosti 14, 2025, wakati wavuvi wakihamisha mafuta ya petroli kutoka kwenye madumu, hali iliyosababisha cheche na kupelekea mlipuko wa moto.
"Chanzo cha tukio hilo ni wavuvi kuhamisha mafuta ya petroli toka kwenye madumu na kusababisha cheche zilizopelekea moto kulipuka. Katika tukio hili hakukuwa na kifo wala majeruhi, katika tukio hilo watu 1000 wamenusurika kifo huku hasara zilizotokana na moto huo ni kuungua kwa stoo moja ya kuhifadhia mafuta ya Petrol na kuteketea madumu mawili yenye lita 500”, ameeleza.
Katika tukio tofauti, mtu mmoja anayedaiwa kuwa na matatizo ya afya ya akili, Nyarali Masungu (52), amefariki dunia baada ya kujifungia ndani ya chumba chake na kuwasha moto kwa kutumia mafuta ya petroli katika Mtaa wa Mazezere, Kata ya Sumve, wilayani Kwimba.
"Tukio la moto wa nyumba ya makazi lililotokea Wilayani Kwimba kata ya Sumve mtaa wa Mazezere na chanzo cha tukio hilo ni Ndugu Nyarali Masangu kujifungia ndani ya chumba chake na kuwasha moto kwa kutumia mafuta ya petroli, inasadikika kuwa alikuwa anasumbuliwa na tatizo la afya ya akili," amesema
Kwa mujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, moto huo uliteketeza nyumba aliyokuwa akiishi, ambapo kati ya vyumba tisa vya maduka vilivyokuwemo, sita viliokolewa.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Mwanza limewataka wananchi wote wanaojishughulisha na biashara au uhifadhi wa mafuta yenye uwezo wa kulipuka, ikiwemo petroli, kuchukua tahadhari na kufuata kanuni za usalama ili kuepusha majanga ya moto.