A
Anonymous
Guest
Mimi ni mdau wa JamiiForums, nipo Mwanza, Wilaya ya Ilemela, Tarafa ya Nyamhongoro, Kata ya Ibwinza.
Kwa muda mrefu tumekuwa tukitegemea kisima kimoja kwa ajili ya kupata maji ya matumizi ya kila siku. Hata hivyo, kwa sasa kisima hicho kimejaa matope na hakifai tena kutumika, jambo ambalo limeongeza ugumu mkubwa kwa wakazi wa eneo hili.
Sio kila mwananchi ana uwezo wa kuchimba kisima chake binafsi, hivyo wengi wetu tumebaki bila chanzo cha uhakika cha maji. Wakati huo huo, mradi wa maji uliopo unaonekana kuishia katika Kata ya Nyamadoke, hali inayotuacha sisi bila huduma hiyo muhimu.
Kutokana na hali hii, baadhi ya wananchi wanalazimika kununua maji kutoka kwa wasafirishaji wa maji kwa kutumia baiskeli, jambo ambalo linaongeza gharama za maisha kwa kiasi kikubwa.
Kwa kweli, changamoto ya maji imekuwa kero kubwa na inatesa wananchi wa eneo hili.
Tunaomba sana uongozi wa Mkoa wa Mwanza pamoja na mamlaka husika kama MWAUWASA kuingilia kati kwa haraka, ili kutuletea huduma ya maji kupitia mabomba na kutupatia suluhisho la kudumu la tatizo hili.