A
Serikali Mwanza ni kama haipo, barabara ni aibu, maji ni kero, kuna maeneo kama usagara umeme tunaambiwa mpaka mtu mzito akamwage hela.Hivi,Mwanza haina viongozi na watendaji katika ngazi za mitaa hadi mkoa?Mwanza inaitwa Jiji lakini kwa hali hii uhalisia wake ni mbuga kubwa wanayoishi binadamu na mambo yake.Je, hakuna ubunifu,mikutano,uibuaji kero na ukabiliano wa kero hizo?Kwenye Jiji,leo hii na karne hii watu wanaomba wapelekewe maji ya visima? Kweli kabisa?
Watu wa Mwanza jiji mmekwama na viongozi wenu ni bure kabisa.Kadhia hiyo ya maji imeanza siku nyingi.Hamkwepi hilo.Sifa mojawapo ya kuwa jiji ni uwezo wa kujipatia huduma za kijamii kikamilifu.Sasa mtatueleza kipi mueleweke?Huu siyo wakati wa maji ya visima wala mabomba ya maji ya jumuiya/magati.Vyanzo vya maji mnavyo,wataalamu mnao,rasilimali vitu mnavyo.Vitumieni kwa ufanisi kuondoa kadhia na kuwa dhalili kiasi hicho.
Ndiyo hivyo?Basi kuna hatari kubwa sana.Mji mkubwa,una mapato mazuri,muundo wa kijiografia mzuri.Tatizo ni kuwa na uongozi na utendaji dhaifu kuliko dhaifu yenyewe.Jiji lililo kati ya nchi zaidi ya tatu,tena ni wadau kamili linajiendesha kama kijiji kipana kando ya nchi.Aibu gani hiyo!?Serikali Mwanza ni kama haipo, barabara ni aibu, maji ni kero, kuna maeneo kama usagara umeme tunaambiwa mpaka mtu mzito akamwage hela.
Serikali ya CCM ituachie jiji letu tukusanye Maputo yetu na kujiletea wenyewe maendeleo