Mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence Melo azuiliwa Tanzania - BBC Swahili

elbarik

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2016
Posts
576
Reaction score
395
Mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence Melo azuiliwa Tanzania
Mwanzilishi wa mtandao maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wa Jamii Forums Maxence Melo anashikiliwa na polisi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jamii Forums Melo anashikiliwa kwa kukataa kutoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo.

Anatarijiwa kufikishwa mahakamani Jumatano asubuhi.

Mwandishi wetu Sammy Awami alizingumza na mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums Mike Mushi na alianza kwa kuelezea mwanzo wa kesi hiyo.


Mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence Melo azuiliwa Tanzania - BBC Swahili
 
"We reserve the right to disclose personal information when needed to comply with the law or a legal process, cooperate with investigations of purported unlawful activities (identified serious crimes), to identify persons violating the law".

If it is not neccessary Mr.Melo atakuwa na haki ya kukataa kutoa taarifa za watumiaji.
 

Whatsapp, FB, Apple na others huwa hawadisclose. The government ya Tz haifaia kupata info ya mtu yeyote anayeutumia huu mtandao.
 
haya ndio madhara ya matamko ya viongozi wetu, wanasahau kwamba wanawatenda kazi wasio fikirisha akili zao kupima mambo na uzito wake. Mtumishi anaposikia mkubwa anasema anatamani malaika waizime mitandao ya kijamii unategemea nini? Tutarajie vurugu endelevu nyingi tu, kama wao kweli wanafanya kazi yao vizuri mbona hawamkamati Mange? Wafunge insta basi tujue wao kweli wamedhamiria.

Kwanini hili limekuja baada ya uvumi wa hivi karibuni aliopost dada yule kuhusu kulazwa kwa mama wa kwanza?
 
Where we dare to talk in deed [emoji2][emoji23][emoji23][emoji23][emoji6]
 
Nakumbuka sakata la DANGOTE lilivyofika BBC kesho yake Rais alilitolea tamko..
Nafahamu na hili nalo litakuwa hivyo hivyo la sivyo atakuwa anakula matapishi yake....
......PAMOJA BBC...
 
Hivi kwanini wasiwasake members moja kwa moja na sio kuwatafuta wamiliki?

Mbona Facebook wanawakamata kupitia akaunti zao? Kwanini hawajawakamata wamiliki?

Basi wakawakamate wamiliki wa Instagram ili wasaidie kukamatwa kwa Mange Kimambi..
 
Hivi kwanini wasiwasake members moja kwa moja na sio kuwatafuta wamiliki?

Mbona Facebook wanawakamata kupitia akaunti zao? Kwanini hawajawakamata wamiliki?

Basi wakawakamate wamiliki wa Instagram ili wasaidie kukamatwa kwa Mange Kimambi..

Huu ni udictator. User information should never be shared. Hata huku Kenya Safaricom haiwezi ipa serikali data ya watumizi kiholela
 
wangejua jamii forum inaelimisha kias gani wala wasingechkua hatua hii
 
Huu ni uhujuma!!! [emoji34] [emoji34]
 
Huu ni udictator. User information should never be shared. Hata huku Kenya Safaricom haiwezi ipa serikali data ya watumizi kiholela

Mbaya sana mkuu. Hii ni aibu kwa taifa linalipigiwa mfano kama muhimili wa demokrasia africa.
 
Walisema Magufuli atosha, kumbe hatoshi mboga. Mimi niko Kenya aisei natazama tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…