Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Julian Assange akipanda ndege maalum kuelekea Saipan
Mwanzishi wa WikiLeaks Julian Assange ameachiwa huru usiku huu kutoka gereza la Belmarsh nchini Uingereza ambako amekaa kwa miaka 12. Bwana Assange alikuwa akikaa gerezani hapo akisubiri kupelekwa Marekani kujibu mashtaka ya ubakaji ambako alikuwa akituhumiwa alifanya nchini Sweden.
Miaka 12 ilopita Julian Assange alikimbilia ubalozi wa Ecuador uliopo nchini Uingereza baada ya tuhuma hizo kutolewa na pia kuwepo kwa tuhuma zingine kutoka Marekani ambayo imekuwa ikimtuhumu kudukua taarifa za siri ambapo video ilionyesha wanajeshi wa Marekani wakifanya uhalifu wa kivita nchini Irak.
Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa na kundi la siri la wadukuaji kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), Assange ameondokea uwanja wa ndege wa Stanstead uliopo mashariki mwa jiji la London na muda si mrefu atakutana na mkewe Stella Assange na watoto wao wawili ambao hwakuwahi kukaa na baba yao nyumbani.
Ndege hiyo itatua mjini Bangkok nchini Thailand kabla ya kuelekea mjini Saipan.
Hapo chini ni barua ya waendesha mashtaka wa Marekani wakielekeza mkutano wao na Juliana Assange mjini Saipan katika kisiwa cha Mariana. Kisiwa hichi chamilikiwa na Marekani na hakipo mbali kutoka nchi Australia ambako Assange alizaliwa.
Vyanzo vya habari hii: Reuters, EPA, AP , CNN na media outlets.
Julian Assange ni nani?
Julian Assange akiwa nje ya jengo la ubalozi wa Ecuador mjini London mwaka 2016. Picha na AP ilochapishwa na gazeti la The Standard.
Julian ni mhariri wa habari za kiuchunguzi, mwanaharakati na pia ni mchapishaji. Alizaliwa nchini Austalia mwaka 1971 na ni mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks ambao ulianza rasmi shughuli zake mwaka 2006.
Julian ameishapokea tuzo kadhaa za uandishi wa habari na uchapishaji lakini ni mwaka 2010 ndipo alipokuja kujulikana kimataifa kwa kazi zake pale mtandao wake wa WikiLeak ulipochapisha nyaraka za siri kutoka Pentagon makao makuu ya jeshi la Marekani.
Nyaraka hizo zilionyesha video zilohusu majeshi ya Marekani kuwaua raia waso na hatia katika nchi za Afghanistani na Irak na pia mateso walokuwa wakiyapata wafugwa wa kigeni katika kambi ya Guantanamo.
Pia mtandao huo ulichapisha mawasiliano mbalimbali ya siri kati ya viongozi wa serikali ya Marekani na nchi zingine kadhaa ulimwenguni ikiwemo taarifa ya mauaji ya kisiasa nchini Kenya mwaka 2008 ambayo yalichapishwa na gazeti la Sunday Times.
Misukosuko dhidi ya Assange ilianza na nchi ya Sweden kutoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Assange ili kupelekwa Sweden kukabili mashtaka ya kumshambulia kimwili mwanamke mmoja wa nchi hiyo. Bwana Assange alijaribu kupinga hati hiyo ya kukamatwa na akashindwa jambo lilomfanya mwezi Juni mwaka 2012 akimbilie ubalozi wa Ecuador ulioko London nchini Uingereza ambako baadae mwezi wa August mwaka huohuo alipata hifadhi ya kisiasa.
Baadae mwaka 2019 nchi ya Sweden aliondoa mashtaka yalomkabili Assange na mwezi April mwaka huohuo Ecuador ikaondoa hadhi ya ukimbizi alokuwa nayo jambo lilowapa uwezo polisi wa Uingereza kuingia ubalozini humo na kumkamata Assange na kupelekwa gereza la Belmarsh akisubiri kupelekwa Marekani kujibu mashataka ya kudukua nyaraka za siri katika mifumo ya kompyuta ya Pentagon kupitia mwanajeshi alieitwa Chelsea Manning ambae alikuwa ni mchambuzi wa ujasusi wa jeshi la Marekani.
Assange ana kipaji cha udukuzi yaani "hacking" ambapo alianza shughuli hizo za udukuzi akiwa na umri wa miaka 16. Mwaka 1988 alitumia uhandisi jamii (kumrubuni mtu ataekusadia kazi) kudukua taarifa kutoka kamisheni ya mawasiliano ya Australia bila kuharibu mifumo yake ya Kompyuta..
Mwaka 1991 gazeti la he Guardian la Uingereza lilimpa sifa ya kuwa mdukuzi aliejitosheleza yaani "The most accomplished hacker" na hadi hapo tayari alikuwa amedukua mifumo zaidi ya elfu moja ikiwemo mifumo ya kompyuta ya Pentagon.
PIA, SOMA:
- Je, Julian Assange ni Shujaa au Msaliti?
- Julian Assange wa WikiLeaks kukiri kosa la kuvunja sheria za ujasusi za Marekani
- Wikileaks: Julian Assange aruhusiwa kufunga ndoa jela
- Mahakama ya Uingereza yahukumu Assange anaweza kurejeshwa nchini Marekani
- Snowden amuomba Trump amuachie Julian Assange kizuizini nchini United Kingdom kabla hajahukumiwa
- Julian Assange: Trump 'offered pardon for Russia denial'