The Mongolian Savage
JF-Expert Member
- Jul 5, 2018
- 8,082
- 17,838
Yani wabongo bana wakishakamata vijichenji kidogo fujooo na kuanza kuringishia.
Aliyekuwa mpambe/mlinzi ama bodyguard wa msanii maarufu nchini Diamond jitu lenye miraba minne Mwarabu fighter naye ameanza kujianika kwenye mitandao ya kijamii na maburungutu ya pesa.
Katika ukurasa wake wa Instagram Mwamba huyo anaonekana akiendesha gari huku akiwa ameweka pembeni kibunda kilichoshen msimbazi za kutosha. Isitoshe pia anaturingishia saa ya dhahabu.
Issa Tambuu bilionea mstaarabu naye Dotto magari alishaanza kumponza akaanza hii tabia mbofumbofu ya kujianika na pesa mtandaoni.
Watu tulisikitika sana kwasababu jamaa ni mtu wa ibada kwanini akufuru? Lakini kutokana na uungwana wake akaomba msamaha na nakuahidi hatarudi tena na kujitetea eti alikuwa anafanya hivyo kuwapa uaminifu wateja wake likija swala zima la pesa.
Tumemsamehe huyu kijana wetu wa Allah mstaarabu Issa.
Ila wabongo ni waajabu wamemuambukiza hadi huyu Mzungu. Wazungu wengi hawanaga hii tabia lakini jamaa huyu Mzungu kaishi na kujichanganya na sisi mibongo na kuambukizwa hii Tabia mbofumbofu. Hapa kwenye ukurasa wake wa FB akijianika na burungutu ya USD.