Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Kumbuka Mwarabu alifika ardhi yetu ikiwa bikra, yani ilikuwa ni misitu na wanyama tu, unaambiwa enzi hizo msitu ulikuwapo hadi hapo kisutu, yani simba walikuwa wapo hadi magomeni, chui wapo hadi kigamboni, papa wapo hadi fukwe za mbezi beach, chatu wapo hadi Msasani, sasa kwa msingi huo national park za nini na ilibidi ardhi itumike kufanya mazingira bora ya kuishi, kumbuka binadamu sio mnyama pori.
Na hili ndio nchi zinazojielewa wanapambana sana kurudisha Hali hiyo na kuishi na wanyama au ndege na viumbe wa bahari
Kuna samaki walipotea kabisa karibu na miji kwa sababu ya watu kuendeleza kelele na fujo baharini na misitu kukatwa miti hovyo hivyo kusababisha wanyama kuhama au kufa pia ndege wengi wamehama pia
Mfano mdogo leo ukienda New York wale dolphin [emoji227] wamerudi kwa kasi kwa sababu wameweka restrictions nyingi sana baharini mpaka sasa na wale humpback [emoji229] wameonekana pia ambapo ni jambo la ajabu sana
Yaani unasimama NY leo unaona Nyangumi
Sasa hata Sisi tunaweza kuwa na hifadhi karibu na tukawapa heshima wanyama kwa kuishi bila bughudha
Kwanza sidhani hata kama kuna takwimu zinaonyesha ni ndege aina ngapi wamepotea Tanzania na kuisha kabisa au hata wanyama aina ngapi wametoweka au kuisha kabisa
Nakumbuka Egypt kuna kasa wadogo walikuwa wanaliwa sana mpaka wakawa extinctions kabisa kasoro tu waliobaki Zoo
Hivyo wazungu wakawaomba wawachukue na kwenda kuwakuza na kuzaliana kwenye hifadhi maalumu
Wamekuwa wengi na kuwarudisha tena Misri